Thursday, June 2, 2016

WILAYA YA ILALA YAJIPANGA KUSAMBAZA MAENEO YOTE MAKASHA YA KUHIFADHIA TAKA

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza wakati wa uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani ambapo manispaa ya Ilala kwa kushirikiana na Kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd na nyingine kwa kufanya usafi katika fukwe za bahari ya Salender jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni na kulia ni Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda.
 
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni akizungumza jambo na wadau wa mazingira waliokusanyika kwenye viwanja vya Salender Club kabla ya kuanza zoezi la usafi wa mazingira.
Baadhi ya wadau wa mazingira kutoka ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, makapuni ya usafi yaliyopewa zabuni ya kusafisha manispaa ya Ilala ikiwemo Green Waste Pro Ltd, Vijana kutoka Roots and Shoot waliokusanyika kwenye uzinduzi wa wiki ya mazingira duniani iliyozinduliwa jana duniani kote.
Kiongozi wa dhehebu la Dawoodi Bohra nchini, Bw. Zainuddin Adamjee (wa pili kushoto) akimtambulisha Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin (wa tatu kushoto) kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (kulia) mara baada ya kuwasili jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine (kushoto) akitoa salamu za serikali kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Bohora duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin aliyewasili jana jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akielezea mipango ya manispaa ya Ilala katika kuweka jiji safi wakati wa hafla fupi ya kukabidhiwa 'Dustbin' 53 zilizotolewa na Burhani Foundation Tanzania iliyofanyika katika mskiti wa dhehebu la Mabohra nchini.
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin moja ya Dustbin kati ya 53 zilizotolewa na Burhan Foundation kwa Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi katika hafla fupi iliyofanyika nyumbani kwa Kiongozi huyo jijini Dar es Salaam.
Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin akimvisha kikoi Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi na kumwombea dua baada ya kukabidhi Dustbin 53 kwa ajili ya manispaa ya Ilala.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akimshukuru Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin kwa zawadi ya kikoi.
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda akipokea zawadi ya kikoi kutoka kwa Kiongozi Mkuu wa dhehebu la Dawoodi Bohra duniani, Ali Qadaar Syedi Mufadal bhaisaheb Saifuddin.
Mwenyekiti wa CCM, Serikali za Mitaa Kata ya Kisutu, Mustaquim Darugar (kushoto) akifurahi jambo na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.

Ikiwa ni wiki ya mazingira duniani, Wilaya ya Ilala imeeleza mipango yake ya kuweka mazingira katika hali ya usafi kusambaza makasha yatakayotumika kuhifadhia taka baada ya kupokea msaada wa makasha 53 kutoka Taasisi ya Burhani.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi alisema wilaya yake imeanza kujipanga katika hilo ili kuweka mazingira safi na kuwataka wananchi wote kutupa taka katika makasha hayo mara tu baada ya kumaliza matumizi yao.

Alisema jukumu la kuweka mazingira katika hali ya usafi nila kila mmoja hivyo kila mtu ana wajibu wa kushiriki kuweka mazingira yanayomzunguka katika hali ya usafi jambo ambalo linaweza kusaidia kuondokana na magonjwa ya mlipuko ambayo mara nyingi yamekuwa yakisababishwa na uchafu uliosambaa katika mazingira yanayotuzunguka.

“Kwa wananchi wote hata kama ukinywa maji au kula embe, ndizi na hata kama ni vocha au umetumia sigara uchafu wote uwekwe katika makasha hayo ili tuweze kuweka wilaya katika usafi na uchafu huo utakuwa unakuja kuchukuliwa na watu ambao tumewaweka kufanya kazi hiyo,

Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda (kulia) akimkaribisha Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati) kuzindua wiki ya mazingira duniani pamoja na kuzungumza na wakazi wa mtaa wa Sea-View pamoja na wafanyakazi wa makampuni ya usafi ikiwemo Geen Waste Pro Ltd. Kushoto ni Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Sea-View Upanga, Victor Muneni.

“Wilaya yetu imejipanga kwa sasa kusambaza makasha katika mazingira yetu na katika kata zote ni wajibu wa kila mmoja kushiriki kuweka mazingira katika hali ya usafi uchafu wote unatoka katika mazingira yetu hatuna budi kushirikiana kufanya usafi,” alisema Raymond.

Kwa upande wa Taasisi ya Burhani ambao ndiyo wametoa msaada kupitia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Mabohra, Muslim Hassuji alisema wametoa msaada huo ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono Rais Magufuli kuweka mazingira katika kusaidia kuweka mazingira safi na pamoja na msaada huo pia wamejipanga kuendelea kutoa msaada wa vifaa katika maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam.

“Tunamuunga mkono Rais wetu Magufuli ili tuweke mazingira yetu safi, msaada huu wa makasha ya kuhifadhia taka 53 kwa wilaya ya 53 ni awamu yetu ya kwanza na tutaangalia jinsi yatakavyofanya kazi na baada ya hapo tutatoa mengine na baadae tugawe hata kwa mkoa wote wa Dar es Salaam,” alisema Hassuji.

Nae Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafi ya Green West Pro Limited, Anthony Mark aliwataka Watanzania wabadilike na kuwa na kujiwekea utaratibu kuweka mazingira yanayowazunguka safi kutokana na wengi wao kujisahau kufanya usafi.
“Watanzania wengi sio wastarabu unakuta mtu yupo ndani ya gari anakunywa hata maji akimaliza anatupa kopo nje hii sio tabia njema inatakiwa ifike hatua tubadilike na tushiriki kuweka mazingira yetu safi sio wengine wanafanya wengine hawashiriki,” alisema Mark.

Aidha Mkurugenzi huyo wa Green West Pro aliwatupia lawama Shirika la Umeme nchini (TANESCO) kwa tabia ya kuacha miti ambayo wamekuwa wakikata kwa madai ya kuwa karibu na nguzo za umeme na baadae kuiacha.

Alisema sio ustaarabu kwani kufanya hivyo ni kuchafua mazingira na kuwaachia wananchi uchafu ambao haukusababishwa na wao na hivyo kuwataka kubadilika ili kusaidia kuweka mazingira safi kama jinsi Rais Magufuli anavyoagiza.

Nae Mkuu wa Idara ya Usafi na Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda alisema kuelekea kilele cha wiki ya mazingira wataendelea kushiriki katika maeneo mbalimbali kufanya usafi ikiwa ni kutekeleza agizo la Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ambapo kwa kuanza hapo jana Jumatano walishirikiana na Kampuni ya Usafi ya Green West Pro ltd ambapo walifanya usafi katika eneo la Salender Bridge.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akitoa maagizo kwa Kamanda wa kituo cha Polisi Salender Bridge kuhusiana usafi wa mazingira kuzunguka maeneo yao katika fukwe za bahari ya Salender.
Mkaazi wa mtaa wa Sea-View mzee Peter Kabelwa almaarufu kama Mzee Mzungu akishiriki zoezi la kuondoa uchafu uliozunguka katika fukwa za bahari ya Salender Bridge.
Mwanamazingira kutoka Roots and Shoots akishiriki kukusanya taka zilizosambaa kwenye eneo la fukwe za bahari ya Salender Bridge.
Mkurugenzi wa kampuni ya usafi ya Green Waste Pro Ltd, Anthony Mark Shayo na Meneja Uendeshaji wa kampuni hiyo, Abdallah Mbena (kulia) wakishirikiana na wafanyakazi wa kamouni hiyo kufanya usafi kwenye eneo la fukwe za bahari ya Salender Bridge.

Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na wadau wa mazingira wakiendelea na zoezi la usafi kwenye fukwe hizo.
Afisa Mazingira kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ilala Bw. Abdon Mapunda (katikati) akishiriki zoezi la usafi kwenye fukwe za bahari ya Salender Bridge.

Eneo hili lilisahaulika kwa muda mrefu bila kufanyiwa usafi kitu ambacho ni hatari kwa samaki wanaoishi kwenye fukwe hizo.
Muonekano wa fukwe za bahari ya Salender Bridge kabla ya kusafishwa na wadau wa mazingira wakiwemo Green Waste Pro Ltd.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akiagana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Usafi ya Green West Pro Limited, Anthony Mark baada ya kuzindua wiki ya mazingira Manispaa ya Ilala ambapo dunia kote inaadhimisha.

No comments: