Friday, June 24, 2016

TASWIRA MBALIMBALI KUTOKA JIJINI MBEYA LEO

 Huu ndio mnara unaolitambulisha Jiji la Mbeya uliopo katika kipita shoto kinachoelekea maeneo ya katikati ya Mji. historia inaonyesha kuwa Mnara huu ulijengwa mnamo Mwaka 1974 ikiwa ni katika Maadhimisho ya Miaka 20 ya kuzaliwa kwa Chama cha Tanu ambacho baadae kilizaa Cha cha Mapinduzi (CCM). Huu ni Mnara maarufu sana Jijini hapa, ukiwa ni moja ya alama muhimu pia.
 Kwa mbali kule ni Mlima Loleza ambao ni moja ya Milima inayoupendezesha sana Mkoa wa Mbeya.
 Uwanja wa Ndege wa Mbeya, sasa magari tu ndio yanajiachia.
 Sifa nyingine kubwa katika Jiji hili ni kutawala kwa ukijani kila kona, maana miti ipo kila mahala.








No comments: