Thursday, June 9, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Serikali imepokea gawio la fedha kiasi cha billioni 23 kutoka kwa makampuni ya NMB TIPPER na PUMA ikiwa ni faida iliopatikana baada ya serikali kuwekeza hisa kwenye makampuni hayo. https://youtu.be/wmLJdj-9QzQ  

SIMU.TV: Shirika la umeme nchini TANESCO limesema changamoto kubwa inayolikabili ni kukosa vyanzo vya maji vya uhakika kwa ajili ya kuzalisha nishati umeme wa uhakika.https://youtu.be/19UYIM4rtp4

SIMU.TV: Mkoa wa Singida umefanya zoezi la kuwatambua madaktari bingwa walioko mkoani humo na kuunda timu ya madaktari bingwa watakaozunguka katika wilaya za mkoa huo kutoa huduma. https://youtu.be/b1cWbtZjsiI

SIMU.TV: Wakulima nchini wameshauriwa kulima kilimo mseto ili kuwawezesha kulinda ardhi pamoja na kuvuna mazao mengi ya aina mbali mabali .https://youtu.be/V_g4sl4dquk

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Mwanza amesema kuna uhutaji wa wahitimu kutoka taasisi ya taaluma ya wanyama pori kutumia mbinu za ziada kuhakikisha wanapambana na ujangili. https://youtu.be/ntalRVC8Yoc

SIMU.TV: Kampuni ya kimataifa ya ushari wa kibiashara ya E&Y imesema ongezeko la silimia 30 kwenye bajeti ya maendeleo itasaidia kukua kwa uchumi wa nchi.https://youtu.be/mxM9P3OR15M

SIMU.TV: Benki ya DTB imezindua tawi jipya la 25 kama njia ya kusogeza huduma karibu na wateja wake sehemu mbali mbali. https://youtu.be/J6sNtCkso2s

SIMU.TV: Idadi ya michango ya wanachama wa bima ya afya kwenye mfuko wa bima ya afya wa AAR imeongezeka kutokana na kuongezeka kwa wanachama katika mfuko huo.https://youtu.be/UE5m4AhbdBg

SIMU.TV: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imezindua kitu kipya ambapo imetenga milioni mia sita kwa ajili ya kutoa zawadi kwa wateja wake.https://youtu.be/9ex3lKLQ1I8

SIMU.TV: Ukosefu wa wa vifaa umeonekana kuwa changamoto kubwa inayokwamisha ukarabati wa uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera. https://youtu.be/FPaNmbnmmPk

SIMU.TV: Timu za UMISETA na UMITASHUMTA za mkoa wa Dar es Salaam zimekabidhiwa vifaa vya michezo kuelekea fainali za taifa mkoani Mwanza. https://youtu.be/oplpVfKu-GQ

SIMU.TV: Mkoa wa mwanza unatarajia kutenga shule tatu zitakazo toa elimu ya michezo katika kuwania nafasi ya kucheza UMISETA ngazi ya taifa. https://youtu.be/fb4emQe--dA

SIMU.TV: Katika fainali kopa Amerika Brazil imetembeza kichapo kwa Haiti kwa kuwafunga magoli saba kwa moja. https://youtu.be/SKdGW2iAzw0

SIMU.TV: Wataalamu wa masuala ya uchumi nchini wamesema pamoja na bajeti kuonesha matumaini zaidi ya bajeti zilizopita lakini haiwezi kubadili maisha ya watanzania.https://youtu.be/pIEWBfXYC2w

SIMU.TV: Serikali imetakiwa kuhakikisha bejeti ya 2016/2017 inalenga zaidi kuangalia wananchi wa kawaida ili kubadilisha maisha yao kiuchumi. https://youtu.be/8eEnuJrmb8k

SIMU.TV: Chama cha wafanyakazi wa sekta ya mawasiliano COTWU kimeisifu bajeti ya serikali na kusema itasaidia wafanyakazi kiuchumi. https://youtu.be/kaXAcSvp9-c

SIMU.TV: Serikali imeanza uchunguzi wa kuusaka mtandao unajihusisha na kusafirisha wasichana nje ya nchi hususani mashariki ya mbali na india na kwenda kuwafanyisha kazi zisizo na staha kama ukahaba. https://youtu.be/EDu7KsxCK7Y

SIMU.TV: Serikali imeazimia kutumi zaidi ya billion mbili katika kuhakikisha inaboresha upatikanaji wa elimu kwa watu wenye mahitaji maalumu. https://youtu.be/FCForYBTXGg

SIMU.TV: Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom imezindua promosheni mpya kwa wateja wake ambapo washindi watajishindia fedha taslimu kutoka Vodacom.https://youtu.be/RsRvr3vhvN4

SIMU.TV: Wakulima binafsi wa zao la tumbaku mkoani Tabora wamelalamikia agizo la serikali la kuwalazimiasha kujiunga na vyama vya ushirika ili waweze kuuza mazo yao.https://youtu.be/igsPN_Q0Oas

SIMU.TV: Leo ikiwa ni siku ya tatu ya mfungo wa Ramadhani bei ya vyakula imekua ya kawaida kutokana na mwezi kuangukia kipindi cha mavuno.https://youtu.be/FX3LTx8_ccw

SIMU.TV: Timu ya ngumi ya JKT imeendela kufanya mazoezi kwa ajili ya mashindano ya meya yatakayo fanyika kuanzia tarehe 21. https://youtu.be/jyo_y4Zt4zk

SIMU.TV: Shirikisho la soka nchini TFF limetakiwa kuthibiti mizengwe na matatizo ya upangaji wa matokeo ili kuwezesha kuondoa migogoro kwenye michezo.https://youtu.be/mhTWfFLfIk8

SIMU.TV: Wafukuza upepo 17 kutoka mkoani Manyara wameondoka katika mkoa huo kwenda kushiriki mashindano ya mchujo wa kuwania nafasi ya kucheza Olimpiki.https://youtu.be/gQl__vEF7BQ

SIMU.TV: Michuano ya EURO inatarajiwa kuanza kesho ambapo timu zaidi ya 30 zinatarajia kuingia katika michuano hiyo kutafuata ubingwa wa nchi za Ulaya.https://youtu.be/BPeXmDxRGHE

No comments: