Saturday, June 11, 2016

MASAUNI ALIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUPAMBANA NA MAJAMBAZI MWANZA, ATOA RAMBIRAMBI KWA WAKE WA WALIOUAWA MSIKITINI.

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani humo, Ahmed Msangi (wa tatu kushoto) pamoja na askari wengine wa jeshi hilo, wakiyaangalia mapango ya utemini, jijini Mwanza ambako kulifanyika operesheni ya kupambana na majambazi baada ya majambazi hao kufanya mauaji katika msikiti wa Rahmani uliopo Kata ya Mkolani jijini humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa pili kushoto) akimuuliza jambo Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kushoto) wakati walipokuwa wanawasili msikiti wa Rahmani mkoani humo uliovamiwa na majambazi na kuua waumini watatu ndani ya msikini huo.
 wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi (kulia) wakati walipokuwa wanatoka msikitini mara baada ya kuzungumza na waumini wa msikiti huo wa Rahmani mkoani humo. Msikiti huo ulivamiwa na majambazi hivi karinbuni na watu watatu waliuawa.
 Mzee wa Msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani, jijini Mwanza, Abeid Gati (kushoto), akimpa fedha mke wa mmoja wa watu waliouawa na majambazi ndani ya msikiti huo. Fedha hizo zilitolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) ikiwa ni rambirambi yake kwa wafiwa wote watatu ambao walipoteza wenza wao katika mauaji hayo. Hata hivyo Naibu Waziri alisema Serikali imesikitishwa na tukio hilo la kikatili na pia jeshi lake lipo makini na linaendelea kulinda usalama wa wananchi na mali zao.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa Kaunda suti) akitoka kukagua nyumba za makazi ya askari Polisi zilizopo katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, nyumba hizo zimetengewa fedha kwa ajili ya kumaliza ujenzi katika mwaka ujao wa fedha. Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimpa pole askari Polisi, Mageni Kaseha aliyepigwa risasi ya mguu na majambazi wakati wa mapambano kati ya polisi na majamabazi hao katika mapango ya utemini, jijini Mwanza. Askari huyo amelazwa katika Zahanati ya Jeshi hilo iliyopo katika Kambi ya Mabatini, jijini humo.
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akizungumza na askari polisi katika Kambi ya Mabatini jijini Mwanza, ambao walipambana na majambazi na kufanikiwa kuwakamata wakati wa operesheni hiyo. Majambazi hayo yalijificha katika mapango ya Utemini jijini humo na ndipo yakavamiwa na polisi mara baada ya kuvamia msikiti wa Rahmani uliopo Mkolani jijini humo na kufanya mauaji. Masauni aliwapongeza askari hao kwa kupambana na majambazi hayo na kuwasisitiza kuwa kazi bado inaendelea wazidi kupambana mchana usiku ili wananchi waweze kuishi kwa amani. 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella kimpa taarifa ya hali ya usalama mkoani humo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wa tatu kulia) wakati kiongozi huyo wa Wizara alipofanya ziara mkoani humo. Katika ziara yake, Masauni alitembelea mapango ya Utemini mkoani humo ambapo mapambano kati ya polisi na majambazi yalifanyika, pia alienda kuuona msikiti wa Rahman uliovamiwa na majambazi, pia alizungumza na wafiwa na baadaye akamaliza ziara yake kwa kuzungumza na askari polisi ambapo aliwapa pongezi kwa kazi nzuri ya kupambana na majambazi hao. 
Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

No comments: