Monday, May 30, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMU.TV: Wabunge mkoani Dodoma wahoji uamuzi wa serikali kuwarudisha nyumbani wanafunzi zaidi 7000 wa chuo kikuu Dodoma waliokuwa wakisoma masomo ya ualimu;https://youtu.be/W_iP_WHw7Ic  

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watu 15 kwa tuhuma za ujambazi na uporaji kwa kutumia silaha katika sehemu mbalimbali;https://youtu.be/6NFEIYGXnH0   

SIMU.TV: Wakazi wa kimara jijini Dar es salaam wamelalamikia kitendo cha kutofanyia marekebisho taa eneo la ubungo kibo kwani hali hiyo inaweza kusababisha ajali;https://youtu.be/JLxWP3A9mJI

SIMU.TV: Serikali imetoa wito kwa wamiliki wa vyombo vya habari nchini kuwapatia mikataba mizuri wafanyakazi wao ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa weledi;https://youtu.be/pSOg3spy81o

SIMU.TV: Baadhi ya wakazi wa maeneo ya Manyoni na Itigi wamelitaka shirika la habari Tanzania kuongeza usikivu ili waweze kusikiliza matangazo vizuri;https://youtu.be/d2kbtCSjX5U

SIMU.TV: Rais Dr Magufuli amemteua jaji Shabani Lila kuwa jaji mkuu wa mahakama ya rufani nchini, huku akimteua Anne Makinda kuwa mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya NHIF; https://youtu.be/sK7FGsJXNE4

SIMU.TV: Maonyesho ya bidhaa za kibiashara ya Travel Market yamezinduliwa leo mjini Arusha huku wananchi wakitakiwa kuongeza ubunifu zaidi katika bidhaa zao;https://youtu.be/cc1gvg8RXmo

SIMU.TV: Mamlaka ya viwanja vya ndege nchini TAA kimeitaka chuo cha Regional Aviation College kianze kufundisha kozi za urubani ili nchi ipate marubani wake yenyewe;https://youtu.be/vq2I_OnK6iE

SIMU.TV: Fahilisi za sekta ya viwanda zimeshuka nchini kutokana na kushuka kwa bei za hisa katika makampuni mbalimbali nchini; https://youtu.be/vv1-O_wEnNA

SIMU.TV: Mauzo ya mchele katika soko la Tandika yameongezeka kutokana na kuongezeka kwa upatikanaji wa bidhaa hiyo msimu huu wa mavuno; https://youtu.be/OeoVg2IUfoA

SIMU.TV: Wamachinga wanaouza bidhaa zao katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi wamelalamikia kushuka kwa mauzo yao kutokana na kupungua kwa wateja;https://youtu.be/awiV6EAf-s8

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya taifa Charles Mkwasa amesema timu ya misri isitegemee mteremko katika mechi yao dhidi ya Stars; https://youtu.be/1A_21WZDsjk

SIMU.TV: Wakuu wa shule za binafsi nchini wameshauriwa kuwaruhusu watoto kushiriki katika michezo mbalimbali ili kuwajengea uwezo mkubwa wa michezo;https://youtu.be/bxiibRMGdgk

SIMU.TV: Timu ya Pan African imetakiwa kufanya uchaguzi haraka iwezekanavyo ili kunusuru kuendelea kwa mgogoro unaofukuta katika klabu hiyo;https://youtu.be/IWk1s8Gl3HM

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maluumu ya Dar es salaam limesema litaendelea kuwasaka watuhumiwa wote wa makosa ya uhalifu ili kuimarisha amani na usalama nchini; ;https://youtu.be/6NFEIYGXnH0

SIMU.TV: Wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania leo bila kujali itikadi zao za vyama wametoka bungeni wakishinikiza bunge kujadili sakata la kufukuzwa kwa wanafunzi wa stashahada katika chuo kikuu cha Dodoma. https://youtu.be/iOfxN-Y9IWE

SIMU.TV: Mkazi waBuguruni Kisiwani jijini Dar es Salaam ametiwa nguvuni baada ya kukutwa na kuku zaidi ya sabini waliokufa ambao alikua akiwaandaa kwa ajili ya kuwauzia wauza chipsi na kwenye migahawa. https://youtu.be/3KL7ufmrnL8

SIMU.TV: Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kukusanya zaidi ya milioni mia tano ikiwa ni tozo na faini kutoka kwa madereva waliovunja sheria za barabarani. https://youtu.be/sG7v9dSPs0I

SIMU.TV: Katibu mtendaji wa Tume ya vyuo vikuu nchini TCU aliyesimamishwa kazi Profesa Yunus Mgaya amekanusha taarifa zilizosambaa kuwa utaratibu haukufuatwa katika kuwapumzisha kazi watendaji wa bodi hiyo. https://youtu.be/SzVOncJ5IU8

SIMU.TV: Wadau wa utafiti wa viashiria na maambukizi ya UKIMWI wamesema kuwa ugonjwa huo bado ni tishio na unarudisha nyuma nguvu kazi ya taifa.https://youtu.be/QVQXx3JV4r0

SIMU.TV: Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania leo amemteua jaji kiongozi Shabani ally Lila kuwa jaji wa mahakama ya rufani ambapo pia amemteua aliyekuwa spika wa bunge Anna Semamba Makinda kuwa mwenyekiti wa bodi ya mfuko wa bima ya afya nchini NHIF. https://youtu.be/zVIOhKJQL6s

SIMU.TV: Halmashauri nchini zimetakiwa kutenda maeneo ya wazi kwa ajili ya uwekezaji na kutimiza azma ya serikali ya kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda na uchumi wa kati.https://youtu.be/0xGP-0GsUEk

SIMU.TV: Jeshi la magereza nchini linahitajika kutafuta kiasi cha shilingi bilioni mbili nukta nane ili liweze kueendeleza mradi wake wa kokoto katika mkoa wa Dodoma.https://youtu.be/1egvsMa1V24

SIMU.TV: Chuo cha usimamizi wa fedha IFM kimeanza kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuweza kuwafanya watanafunzi wanaohitimu elimu ya juu kujiajiri na kuepuka kutegemea kuajiriwa tu. https://youtu.be/Ict15jVkEj8

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kwamba mchezo ujao kati Taifa stars na Misri utakua kama fainali ya kuamua ni nani aende kucheza fainali za bara Afrika. https://youtu.be/puJ_U1oywA4

SIMU.TV: Licha ya kuwepo kwa ligi mbalimbali nchini za kuibua vipaji vya soka lakini kumekua hakuna mpango wa kuendeleza vipaji hivyo ili viweze kunufaisha sekta ya michezo. https://youtu.be/sitL1UdC1QM


SIMU.TV: Serikali imesema ina dhamira ya dhati ya kuinua na kuendeleza vipaji vya michezo kwa wachezaji wachanga ili kuwawezesha kuifanya michezo kuwa ajira.https://youtu.be/KHi9DJ9ZG6s

SIMU.TV: Michuano ya kombe la mkuu wa majeshi CDF imeendelea jijini dare s salaam ambapo timu ya JKT leo imeibuka mshindi dhidi ya timu ya Faru.https://youtu.be/lqeUE_NkhQY

SIMU.TV: Mwanasoka wa mexico aliekua ametekwa nyara amefanikiwa kuokolewa kwa juhudi za  jeshi la polisi nchini humo. https://youtu.be/sokKe8qVVP0

No comments: