Tuesday, May 10, 2016

PSPF YATOA MSAADA WA VIFAA VYA KUSOMEA KWA WANAFUNZI WAISHIO KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MIKOA YA MWANZA NA GEITA

Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani akiwaelimisha wanafunzi wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyoko mkoani Geita kuhusiana na Mfuko wa Penseheni wa PSPF na lengo la kusaidia jamii katika hususan katika masuala ya elimu. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Wanafunzi wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza wakifurahia msaada uliotolewa na PSPF kwa wanafunzi waishio katika mazingira magumu shuleni hapo.
 Afisa Uhusiano wa PSPF, Bibi Coleta Mnyamani ,akiongea na kamati ya shule ya Msingi Igaka (ambao hawapo pichani) pamoja na wanafunzi kuhusiana na lengo la Mfuko wa Pensheni wa PSPF kusaidia jamii hasa kwenye nyanja ya elimu nchini.
Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Wanafunzi waishio katika mazingira magumu wa shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema wakipokea msaada wa mabegi yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Afisa Uendashaji wa PSPF Mkoa wa Geita, Bw. Noel Tuga, akiwapa maelezo wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya msingi Nyansalwa namna ya kutumia vifaa vilivyopo kwenye mabegi PSPF iliyotoa msaada. Mabegi yenye vifaa vya kusomea yalitolewa na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kama msaada kwa wanafunzi waishio kwenye mazingira magumu wa shule ya Msingi Nyansalwa iliyopo Mkoani Geita.
Mwanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka, Bw. Jumanne Masumbuko, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake kwa masaada wa mabegi ya shule yenye vifaa vya kusomea kutoka Mfuko wa Pensheni wa PSPF.
Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Mwanza, Bw. Salim Salum, akitoa rai kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi Igaka iliyopo Wilayani Sengerema Mkoani Mwanza kusoma kwa bidii ili kuinua kiwango cha elimu na kuja kulitumikia Taifa katika siku za baadaye.

No comments: