Saturday, April 16, 2016

YANGA YASHIKA USUKANI WA LIGI KUU, YAICHAPA MTIBWA SUGAR 1-0

 Mshambuliaji wa Yanga, Haruna Niyonzima akitafuta mbinu za kumtoka beki wa Mtibwa Sugar, Majaliwa Shaban katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijii Dar es Salaam. Yanga imeshinda 1-0 na kufikisha pointi 59 na kuongoza katika msimamo wa Ligi huku ikifuatiwa na Simba yenye Pointi 57. (Picha na Francis Dande)
 Mshambukiaji wa Yanga, Thaban Kamusoko akitafuta mbinu za kuwatoka wachezaji wa Mtibwa Sugar.
 Kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed akiokoa moja ya hatari langoni mwake.
 Donald Ngoma akipiga kwa kisigino huku akizongwa na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicenti.
 Hapo je utaweza......
Mshambuliaji wa Yanga, Malimi Busungu (kulia) akitafuta mbinu za Henry Joseph  katika mchezo wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Henry Joseph akichuana na mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe (kushoto).
 Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akichuana na beki wa Mtibwa Sugar, Andrew Vicent
 Henry Joseph akipeana mkono na kocha msaidizi wa Yanga, Juma Mwambusi.
 Kocha na wachezaji wa Yanga wakitoka uwanjani baada ya kumalizika kwa mchezo.
 Haruna Niyonzima akibadilishana mawazo na Simon Msuva baada ya mchezo kumalizika.
 Kocha wa Yanga, Mecky Maxime kulia akiwa na msaidizi wake Zuberi Katwila.
 Kikosi cha mtibwa Sugar kilichoanza leo
 Kikosi cha Yanga kilichoanza leo.

 Deus Kaseke akiwatoka mabeki wa Mtibwa Sugar.
Simon Msuva akimtoka beki wa Mtibwa Sugar.

No comments: