Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu (katikati), akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 255 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa pili kushoto), kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha mawasilianio ya Jeshi la Polisi. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Simon Siro, Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji wa Utekelezaji wa Miradi, Omary Issa (wa pili kulia) na kushoto ni Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Esther Kitoka.
(Picha na Francis Dande)
(Picha na Francis Dande)
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP, Irnest Mangu (katikati) akionyesha furaha yake baada ya kupokea mafano wa hundi yenye thamani ya shs. Milioni 55.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza katika hafla hiyo.
Baadhi ya wageni waalikwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza kabla ya kukabidhi hundi ya Shs. Milioni 255 kwa Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, Inspekta Jenerali, Ernest Mangu akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mfano wa hundi yenye thamani ya shs. milioni 255 kutoka Benki ya CRDB kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa kituo cha mawasilianio ya Jeshi la Polisi.
Meza Kuu.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya CRDB.
Na Glory Chacky.
BENKI ya CRDB imekabidhi msaada wa sh.Milioni 255 kwa Jeshi la polisi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mawasiliano.
Akizungumza jana jijini Dar es salaam wakati wa makabidhiano hayo Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei amesema kuwa wanatambua kuwa jeshi la polisi ili waweze kufanya kazi kwa ufanisi linahitaji mfumo bora wa mawasiliano kati yake na raia.
Alisema wameamua kuelekeza msada huo kwa jeshi la polisi kwa kutambua na kuthamini kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo ya kuhakusha kwamba kuna usalama na amani kwa raia.
Kimei alisema juhudi za wanachi katika kujikwamua katika umaskini hazitafanikiwa kama kutakuwa na ukosefu wa usalama wa raia na mali zao kwa ujumla.
Naye mkuu wa Jeshi la polisi IGP, Ernest Mangu alisema kuwa wanashukuru kwa msaada huo kwani itasaudia kupunguza matukio ya kiualifu.
“ Kituo hiki kitasaidia kulisogeza jeshi la polisi karibu zaidi na wananchi na kushirikiana nao katika kutaarifiana juu ya maswala ya kiualifu pindi yanapojitokeza”alisema Mangu.
No comments:
Post a Comment