Wednesday, February 10, 2016

MKOA WA DODOMA WAZINDUA RASMI KAMPENI YA UGAWAJI VYANDARUA FEBRUARI 9, 2016.

 Kikundi cha ngoma za asili ya kigogo cha Chamwino Ikulu Dodoma kikitumbuiza wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Mkoa wa Dodoma ya kugawa vyandarua vya bila malipo kwa kaya Februari 9, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akigawa vyandarua vya bila malipo kwa wananchi wa kijiji cha Chamwino Ikulu wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.
 Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwafundisha wananchi wa Chamwino Ikulu namna bora ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa kuwalaza kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua Mkoani humo Februari 9, 2016.
 Waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua vya bila malipo wakifuatilia onesho alilolifanya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma (hayupo pichani)la namna bora ya kuwakinga watoto dhidi ya mbu na malaria kwa kuwalaza kwenye vyandarua.
 Maafisa wa Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Dodoma wakiwaonesha Wananchi wa Chamwino Ikulu namna bora ya kujikinga dhidi ya mbu na malaria kwa kulala kwenye vyandarua wakati wa uzinduzi wa kampeni ya ugawaji vyandarua vya bila malipo Mkoani humo Februari 9, 2016.
Wananchi wa mitaa mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma wakiwa wamejipanga kwenye mistari ya kusubiria kugawiwa vyandarua vya bila malipo Februari 9, 2016.

No comments: