Saturday, January 2, 2016

TIMUATIMUA YATUA MNADA WA PUGU, MWIGULU ASHIRIKIANA NA MAWAZIRI WAWILI KUTATUA KERO MACHINJIO YA PUGU

Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa ameambatana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Simbachawene wakiwasili kwenye eneo la machinjio ya Vingunguti kwaajili ya kutoa majawabu kutokana na kero mbalimbali zinazowakabili wadau wa machinjio hayo.
Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Simbachawene wakikagua eneo la machinjio ya Vingunguti kabla ya kuzungumza na wadau wa eneo hilo pamoja na uongozi wake.
Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa ameongozana na Mhe. Simbachawene wakielekea kuzungumza na wananchi wanaotumia Machinjio ya vingunguti.
Mawaziri kutoka kulia ni Naibu waziri wa Afya Mhe. Dkt Hamisi Kigwangallah,Wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa Jimbo la Segerea Mhe. Bonah Kalua,Watatu kutoka kulia ni Mhe. George Simbachawene na wa mwisho kushoto ni Mhe. Mwigulu Nchemba wakijadiliana jambo.
Mkutano ukiendelea wa kutoa majawabu kuhusu changamoto za Machinjio ya Vingunguti.
Mhe. Simbachawene akiwaagiza watumishi wote wa Machinjio ya Vingunguti kuripoti ofisini kwake Jumanne wakiwa na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala.
Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi(Wadau) wa machinjio ya Vingunguti kuhusu hatua za kinidhamu alizozichukua kwa Mkuu wa mnada wa pugu inakotoka mifugo kabla ya kufika Machinjio ya Vingunguti kwa upotevu wa mamilioni ya shilingi ya kodi za serikali.
Mawaziri wakiagana na wananchi mara baada ya mkutano wa kutatua kero zao za Machinjio kumalizika.
Furaha ya Wananchi mara baada ya kutatuliwa kero zao kwa hatua za awali,wananchi wanasukuma gari la Mhe. Mwigulu Nchemba kama ishara ya kukubali hatua alizochukua.
Ile kauli ya HAPA KAZI TU imeendelea kutumika vizuri kwa mawaziri wa Rais Dkt. John  Pombe Magufuli kufuatia  tukio la mawaziri watatu kufika eneo la Machinjio ya Vingunguti kwa ajili ya kutatua kero zinazowakabili wananchi wanaotumia eneo hilo kwa shughuli za kuchinja mifugo.
Awali,Mh.Mwigulu Nchemba alifanya ziara ya kushitukiza usiku wa tar 01/01/2016 katika machinjio hayo na kukutana na madudu ya kutafunwa kwa fedha za ushuru unaokusanywa kwenye mifugo, lakini pia hali ya mazingira ya kutoridhisha ya Machinjio hayo.
Hii leo mapema majira ya saa 3:asubuhi, Mhe. Mwigulu Nchemba amerejea tena kwenye machinjio hayo akiwa ameongozana na mawaziri wawili ambao ni Mhe George Simbachawene(TAMISEMI) na Mhe Dkt. Hamisi Kigwangallah(AFYA) ambao wote wanagushwa na machinjio hayo.
Mara baada ya kusikiliza kero na maoni ya pande zote mbili,Mawaziri hao waliamua kuchua hatua zifuatazo kwa wahusika.
Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza Mkuu wa mnada na watumishi waliokuwa zamu tarehe  24/12/2015 na tar 01/01/2016 watafute kazi nyingine kuanzia sasa, na vilevile wahakikishe Jumatatu wanafika ofisi ya Katibu Mkuu wizara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi.
Pili, Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza kuanzia sasa amesitisha ukusanyaji wa ushuru kwenye eneo la mnada wa Pugu,badala yake makusanyo yote yatafanyika eneo la machinjio la Vingunguti kwa kutumia mashine za kielektroniki za EFD.
Tatu, Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza wananchi kuanzia leo waanze kutumia eneo lililokuwa limetengwa kwa ajili ya kutunzia nyama. Eneo hilo awali lilisitishwa bila sababu maalum na umeme ukakatwa. Mhe. Mwigulu Nchemba ameagiza umeme urudishwe hii leo na wananchi waanze kutumia eneo hilo.
Wakati huohuo,Waziri wa TAMISEMI Mhe Simbachawene ameagiza watumishi wote wa machinjio hayo kujitathimini na kufika Jumanne waripoti ofisini kwake wakiwa na Mkurugenzi wa Manispa ya Ilala kwa ajili ya hatua Zaidi.
Mhe. Simbachawene ameenda mbali zaidi kwa kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala kuhakikisha fedha zinazokusanywa kwenye machinjio hayo zinatumika haraka kujenga miundombinu ya eneo hilo ilikuendana sambamba na wingi wa watu wanaotumia machinjio hayo.
Kwa upande wa Afya, Naibu waziri wa Afya Dkt. Kingwangallah ameagiza daktari wa machinjio hayo Ndg. Juma aache kutoa huduma eneo hilo hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Pia upimaji wa afya kwa wanaotumia machinjio hayo uwe wa bure na uongozi wa machinjio utenge ofisi maalum ya kupima watu hao.

No comments: