Tuesday, January 19, 2016

SIMU TV: UCHAMBUZI WA HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI

Afisa elimu wilaya ya Chamwino Dodoma adaiwa kumpiga makofi hadharani mwalimu wa shule ya msingi kwa kosa la kuchelewa katika semina. https://youtu.be/29ak1Lpkwiw

Watoto wanaoishi katika mazingira magumu Iringa wameonyesha wasiwasi wao kuwa baadhi ya vijana wanaoishi na wazazi wao hawazingatii suala la elimu kutokana na kutegemea mali za wazazi. https://youtu.be/I9vBvwC-t_c    

Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu amezindua matandao utakaoiwezesha serikali kutambua hatua na sheria za ushirikino zinazofanywa na sekta binafsi.   https://youtu.be/ozEretF22-4

Kikosi cha Zima moto na uokoaji katika manispaa ya Bukoba kimewataka wananchi kuchukua tahadhari  kwa kuwa na vifaa vya kuzimia moto majumbani na maofisini ili kuzuia majanga ya moto. https://youtu.be/vQBH6d8OdHE

Serikali imeutaja mkoa wa Mbeya kuwa ndio utakuwa wa kwanza nchini kuanza uzalishaji wa umeme wa  joto ardhi.   https://youtu.be/WJx6ASREnnQ

Mabanda 186 yaliyojengwa na wakazi wa bonde la mkwajuni jijini Dar es Salaam yamebomolewa yote huku wakazi hao wakidaiwa kuondoka katika eneo hilo kabla ya hatua zaidi za kisheria kuchukuliwa. https://youtu.be/8i1DFB8NOKE   

Viwanda viwili mkoani Morogoro vimetozwa faini ya shilingi Mil. 40 kutokana na ukiukwaji wa kanuni za sheria za mazingira.  https://youtu.be/9mmNV73F7VA

Mfuko wa taifa wa bima ya Afya NHIF wazindua kampeni ya kuandikisha wanachama wapya wa mfuko wa jamii mkoani Lindi.   https://youtu.be/fClr8qFD1PU

Makamo wa rais Mhe. Samia Suluhu amezitaka kampuni na taasisi binafsi kuungana na serikali ya wamu ya 5 katika kupiga vita rushwa.   https://youtu.be/GP7LWqdcrFg

Jeshi la polisi mkoani Geita limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa 32 wanaodaiwa kuhusika na mtukio mbalimbali ya kihalifu; https://youtu.be/oKFUyUexiGg

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali itafungua viwanda vya kusindika  ngozi katika mikoa  ya Gieta,Shinyanga na Dar es Salaam; https://youtu.be/6xK9yXxGBEw

Rais John Magufuli aombwa kuingilia kati mgogoro wa viwanja ulipo katika eneo la Mabwepande jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/TO257bo83g0

Mwili wa aliyekuwa mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya CHADEMA, Marehem Leticia Nyerere unatarajiwa kuzikwa siku ya alhamis mkoani Mara;https://youtu.be/AjUpYYv4HVk

Baadhi ya wakulima wa zao la Zabibu mkoani Dodoma waiomba serikali kuruhu uwekezaji wa viwanda vidogo ili kukuza soko la zao hilo;https://youtu.be/TfPCe1DLlWU

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF lajitapa kuwa shirikisho bora la mpira wa miguu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati; https://youtu.be/f1EO6Aw3rWo

Mkurugenzi wa zamani wa klabu ya Bayern Munich, Uli Hoeness anatariwa kuachiwa huru kutoka gerezani mwezi wa pili mwaka huu; https://youtu.be/GWdV7UXxFR0

Waziri wa ujenzi Prof Makame Mbarawa aiagiza mamlaka ya bandari Tanzania TPA kuongeza kasi katika ukusanyaji ushuru; https://youtu.be/4HgxRZn09qM

Shirika la maendeleo ya petroli nchini TPDC linatarajia kujenga kiwanda cha mbolea  wilayani Kilwa mkoani Lindi; https://youtu.be/-bBZXxNx4fE

Serikali yawapiga marufuku watumishi wa umma kutumia anuani binafsi za barua pepe kwa kazi za serikali; https://youtu.be/68w7LLYLWiY

Wananchi wilayani Kaliua waiomba serikali kuisajili shule yao ya  sekondari  walioijenga kwa nguvu zao ili kuwaondolea usumbufu watoto wao kutembea umbali mrefu kutoka katika makazi yao; https://youtu.be/3nChUKauKKk

Serikali ya Israel imewaalika wafanyabiashara kutoka Tanzania kushiriki katika kongamano la biashara litakalofanyika mjini Tel Aviv; https://youtu.be/m_5pCTulikE

Shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF limesema halijapata ombi lolote kutoka klabu ya Simba kuhusu kocha msaidizi wa Taifa Stars Hemed Morocco kwenda kuinoa klabu hiyo; https://youtu.be/9JyRwlvFUj0

Baraza la sanaa Tanzania BASATA lavitaka vyama vya mashirikisho ya wasanii nchini kufanya uchaguzi wa viongozi wao ili kupata viongozi sahihi;https://youtu.be/VR3X025kKIM

No comments: