Monday, January 4, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka watendaji wa serikali kuwajibika vilivyo ili kuendana na kasi ya maendeleo;https://youtu.be/BPXgVvqU5bA  

Mbunge wa jimbo la Kinondoni Mhe. Maulid Mtulya awasilisha pingamizi mahakamani kuhusu zoezi la bomoabomoa katika jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam; https://youtu.be/w-UYdCc6CeM  

Wataalam wa sekta ya ardhi mkoani Mbeya wametakiwa kuwa makini katika upimaji wa ardhi mkoani humo ili kuepuka migogoro isiyo ya lazima;https://youtu.be/H8yFCEdLzPU  

Uongozi wa halmashauri ya Busekelo mkoani Mbeya umewataka  wawekezaji wa kitazania na wale wa kutoka nje ya nchi kwenda kuwekeza katika halmashauri hiyo https://youtu.be/nTj8amcq8o4   

Bondia Francis Cheka wa Tanzania anatarajia kupanda ulingoni kuzichapa na bondia kutoka Uingereza katika kuwania ubingwa wa mabara;https://youtu.be/oL2uMjNHGIw   

Kocha wa klabu ya Liverpool Jurgen Kloop apandisha hasira kufuatia klabu yake kupoteza mchezo wake dhidi ya West Ham United kwa kipigo cha jumla ya magoli 2 kwa bila; https://youtu.be/FC96Gs6XJYM  

Zaidi ya kaya 150 mkoani Mtwara hazina mahala pakuishi huku watu 7 wakijeruhiwa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha mkoani humo;https://youtu.be/e5iQcFs7sBw  

Shirika la Reli TRL limepewa siku tatu kukamilisha ukarabati wa miundombinu ya Reli katika eneo la Magulu mkoani Morogoro;https://youtu.be/laGLFIUzXDM  

Inaripotiwa kuwa wananchi wa wilaya ya Tunduma wako hatarini kupatwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na taka kujaa karibu na makazi yao;https://youtu.be/_4mkRGQV9DQ
  
Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM, Abdallah Bulembo amewataka wananchi kuunga mkono juhudi zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano;https://youtu.be/O7m4LkUwGa4  

Baadhi ya wakazi wa mtaa wa Mgombani Segerea jijini Dar es Salaam wamelalamikia kung’olewa kwa vibao elekezi vya mitaa;https://youtu.be/ATex1XZPqJ4   

Timu ya Yanga imeanza vyema michuano ya kombe la mapinduzi kwa kuitandika timu ya Mafunzo kwa jumla ya magoli 3 kwa 0;https://youtu.be/NasDHROivb0  

Rais wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Dr.Shein azindua maadhimisho ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushiriki zoezi la usafi.https://youtu.be/SzZDQyLGn0E  

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara zaendelea kuleta maafa makubwa baada ya kujeruhi na kubomoa nyumba wilayani Tandahimba.https://youtu.be/P6dHcEnqgL8  

Zikiwa zimebaki siku 3 kabla ya kurejewa kwa zoezi la bomoa bomoa lililositishwa hapo awali jijini Dar es salaam, taharuki yaendelea kuwakumba wananchi ambao nyumba zao zimewekewa X. https://youtu.be/6ERCEsFBW44  

Kasi ndogo ya ujenzi wa Stendi kuu ya Mabasi Songea mkoani Ruvuma yawapa wasiwasi wafanyabiashara waliohamishwa kwa muda kupisha ujenzi huo baada ya kudai kwamba mali zao ziko hatarini kuuzwa na taasisi za fedha kutokana na mikopo waliyochukua. https://youtu.be/ohc-AzPDQ5w  

Mpango wa serikali wa kunusuru kaya maskini umeanza kubadili fikra za baadhi ya wananchi mkoani mkoani Simiyu baada ya kutumia fedha hizo kufanya maendeleo. https://youtu.be/mRR_wZfjiqU  

AZAM TV: Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa aanza ziara yake ya kikazi mkoani Ruvuma na kusomewa taarifa ya mendeleo ya mkoa huo.http://simu.tv/3ERcvoC  

Mbunge wa Kinondoni aishauri serikali kusitisha zoezi la bomoa bomoa na badala yake kuitaka serikali kuwajibika kwa kuwatafutia wananchi hao makazi mbadala. https://youtu.be/_SPgP4kKEtc  

Baadhi ya wataalamu wa sekta ya kilimo waiomba serikali kuipatia kipaumbele sekta hiyo kwa kutoa ajira kwa wingi kwa wataalamu wa kada hiyo kitu kitakachosaidia kuwajengea uwezo wakulima na hatimaye kuondokana na umasikini. https://youtu.be/i5FnAXypAcw   

Waathirika wa dawa za kulevya mkoani Tanga waiomba serikali kuchangia kuwapa huduma muhimu katika vituo wanavyohifadhiwa ili waondokane na matumizi ya dawa za kulevya. https://youtu.be/wTPgMQ2MCSs  

Viongozi wa dini ya Kiislamu mkoani Iringa watakiwa kuhubiri nidhamu kwa waumini wao ili kuepukana na matendo yanayokindhana na maadili.https://youtu.be/VPklfVDkWoo  

Ukatili dhidi ya watoto mkoani Geita wazidi kushamiri baada ya matukio 4 kutokea ndani ya juma moja huku polisi ikibainisha kifo kutokana na matukio hayo. https://youtu.be/sPDQavgY4T4  

Serikali mkoani Njombe yazindua mfuko wa afya ya jamii CHF kwa watoto yatima waishio kwenye mazingira magumu na hatarishi.https://youtu.be/cP4bZCqcTQ0

No comments: