Wednesday, January 13, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI

Serikali yapiga marufuku uuzaji na ubadilishaji wa fedha katika maeneo yasiyo rasmi; https://youtu.be/ZofhQ0bxLHc

Waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe. William Lukuvi asema wilaya ya Bagamoyo inaongoza kwa uuzwaji  holela wa ardhi;https://youtu.be/MqHPWWN5Ur0

Wananchi mkoani Iringa wameutaka uongozi mkoani humo kuimarisha miundombinu ili kuepuka athari zitokanazo na mvua; https://youtu.be/eLpPH1-Phz0

Mkuu wa mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza amemuagiza mkuu wa wilaya ya Tanga kusimamia malipo ya vibarua wa bandari ya Tanga ili waweze kulipwa sawa na maagizo ya serikali; https://youtu.be/6NWl-xgdKkU

Inaelezwa kuwa pato la taifa la Tanzania laongezeka zaidi kwa asilimia 6.3 katika kipindi cha januari hadi septemba 15 kwa mwaka 2015;https://youtu.be/L2vQq4xvlnw

Kocha wa timu ya Yanga, Hans van Pluijm amekanusha uvumi ulioenea kuwa wachezaji wa timu hiyo waligoma kupiga penati wakati wa mchezo baina ya Yanga na URA; https://youtu.be/U__bPMFDlmI

Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemtembelea na kumpa pole mama Maria Nyerere kwa kufiwa na mkwewe marehemu Leticia Nyerere;https://youtu.be/oQqjSIzlDDA

Mtoto mmoja wilayani Geita auawa kwa kuliwa na mamba alipokuwa akifua nguo pembezoni mwa ziwa Vickitoria; https://youtu.be/-SeHtc5ngUo

Serikali mkoani Dodoma imesitisha zoezi la ubomoaji vibanda katika soko kuu la Majengo mpaka pale itakapotoa maeneo mengine kwa ajili ya kina mama lishe;https://youtu.be/cFCnLoPFITM


Mahakama ya Kisutu ya jijini Dar es Salaam imeitupilia mbali kesi iliyofunguliwa na mkazi wa Dar es Salaam,Elias Newala kuhusu kuzuia kwa muda uchaguzi wa mameya kwa manispaa ya Ilala na Kinondoni; https://youtu.be/ULrEM_fJAPQ


Serikali imesema itaanza kuwatoza kodi wamiliki wa nyumba za kupanga katika kuongeza pato la taifa; https://youtu.be/P2SOBtGFAHs

Serikali yalishauri shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF kumtengenezea kumbukumbu mshindi wa tuzo ya mchezaji bora Afrika, Mbwana Ally Samatta;https://youtu.be/BpgbTmBij3w

Siku kadhaa baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Lionel Messi aonekana uwanjani akifanya mazoezi kwa ajili ya mchezo baina ya Barceleona na Espanyol; https://youtu.be/87npHdCQNWY

Waziri ardhi William Lukuvi aagiza manispaa ya Ilala kuvunja jengo la ghorofa 16 baada ya kubainika kuwa na kasoro nyingi. https://youtu.be/Fs82TmS9KjQ

CH10:Mtoto mmoja wa kata ya Nyambonge mkoani Geita afariki dunia baada ya kuliwa na mamba wakati akiosha vyombo katika mwambao wa ziwa Victoria.https://youtu.be/8P2XDu3Fe20


Chama cha mpinduzi CCM chasisitiza kwamba ajenda ya kupinga ufisadi na rushwa nchini kama inavyotekelezwa na Rais Magufuli ni ya chama hicho kinyume na madai ya vyama vya upinzani. https://youtu.be/AVEJ3YygUnQ


Pato la taifa laelezwa kuendelea kukua katika kipindi cha mwezi Julai na  Septemba 2015 kwa kasi ya asilimia 5.3. https://youtu.be/E8GKIF0kcp4


Mwenyekiti wa chama cha watu wenye ulemavu wa ngozi aitaka serikali kufanya uchunguzi kuhusiana na kupotea kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi. https://youtu.be/A_mqgydBDOM

Jeshi la polisi la Dar es salaam latoa onyo na tahadhari kwa watumishi wa benki wanao kula njama na majambazi ili kuvamia na kupora wateja wanaochukua fedha katika benki hizo. https://youtu.be/uf6Ju5MZmNA


Chama cha mapinduzi CCM, chajitokeza na kuipinga Chadema juu ya ajenda ya ufisadi na rushwa huku kikimkalia kooni Tundulisu.https://youtu.be/F2GoyzJ4eUQ


Waziri wa nishati na madini Prof.Sospeter Muhongo aiagiza kampuni ya uchimbaji wa makaa yam awe ya Ngaka TANCO kukaa meza moja na Tanesco na kukubaliana gharama za kuuziana umeme kwa bei nafuu.https://youtu.be/nzTpg9twIHk


Chama cha walimu mkoa wa Dodoma chaiomba serikali kutatua changamoto zinazowakabili walimu wanaostaafu ikiwemo kutowarudisha makwao wanapostaafu. https://youtu.be/XK-zUBBlPGk


Baraza la waislamu Tanzania BAKWATA, lasema kuanzia sasa shughuli zote za UMRA ama HIJJA ndogo zitakuwa zinaratibiwa na baraza hilo.https://youtu.be/VB-dE6Vpl0A


Bodi ya mikopo ya wanafunzi ya elimu ya juu hapa yaelezwa kuvuka malengo ya utoaji mikopo toka uanzishwaji wake. https://youtu.be/7Agi-R87fZk
  
Waendesha bodaboda jijini Dar es salaam wafanya maandamano kuelekea kwa mkuu wa mkoa ili kutoa kilio chao cha kunyanyaswa na askari wa usalama barabarani. https://youtu.be/VVXJLu0tj30

 Bunge la jumuiya ya Afrika mashariki lauvalia njuga mgogoro wa Burundi huku likipokea maaombi maalum kutoka kwa wananchi wa Burundi.https://youtu.be/xGRbjeRXJvA

SIMU.TV: Uhaba wa makocha na ukosefu wa vifaa vya mpira wa magongo waleta changamoto za ukuwaji wa mchezo huo nchini;https://youtu.be/HiGlkV42oaQ  
SIMU.TV: Wakazi wa mkoa wa Iringa wameaswa kupanda miti ili kuzuia maafa yanayotokana na ongezeko la kiwango cha mvua za upepo;https://youtu.be/DGTpGP4H99A  
SIMU.TV: Tume ya taifa ya nguvu ya atomiki yaanza zoezi ya upimaji wa kiasi cha mionzi kinachozalishwa na mtambo wa radar ya mamlaka ya hali ya hewa uliosimikwa mlima Kiseke mkoani Mwanza; https://youtu.be/Ou_66kLPmcQ  
SIMU.TV: Jumuiya ya kusaidia jamii  Zanzibar inaendesha kambi ya matibabu katika kijiji cha Mbuyu tende ili kuboresha afya za wakazi wa wakazi wa kisiwa hicho;https://youtu.be/bRWyuiKsTyc  
SIMU.TV: Klabu ya Coastal Union mkaoni Tanga yamtangaza Ali Jangalu kocha mpya wa klabu hiyo.https://youtu.be/RyGEhZ8-1t8  
SIMU.TV: Wakazi wa Shinyanga wamejikuta katika wakati mgumu baada ya maeneo wanayoishi kuathiriwa na mvua kutokana na miundombinu mibovu ya mji huohttps://youtu.be/kkoobkJ_uQo  
SIMU.TV: Jiji la Dar es Salaam bado linakabiliwa na changamoto ya usafi licha ya agizo la rais la kuhakikisha usafi   nchini nzima; https://youtu.be/ezOEF73fwdU  
SIMU.TV:  Walimu wastaafu mkoani Dodoma wameitaka serikali kuharakisha malipo ya mafao yao yaliyodumu kwa muda mrefu ili kuwapunguzia ukali wa maisha;https://youtu.be/xZKR6k2NW80 
SIMU.TV: Serikali mkoani Lindi imepongeza juhudi zas taasisi binafsi katika kusaidia kuboresha huduma za afya katika jamii; https://youtu.be/9ANC4vqZy6g

No comments: