Wednesday, December 16, 2015

WAZEE TAFF WAMWOMBA WAKIFAMBA AGOMBEE TENA NAFASI YA URAS

Msemaji wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Ahmed Olotu (mzee Chilo) akisoma waraka wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba kwa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile.
 Mzee wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Hamisi Kagaye (kushoto) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo. Kulia ni Mzee Ramadhani Ditopile. 
 Mmoja wa wazee wanaounda Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) Bi. Salome Nonge (kulia) akichangia mada wakati wa kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Bwana Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). Kushoto ni Mzee Ramadhani Ditopile na Mzee Ahmed Olotu maalufu kama mzee Chilo.



Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia tamko la Wazee wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) lililohusu kupinga uamuzi wa Rais wa Shirikisho hilo Simon Mwakifwamba wa kutogombea tena nafasi ya Urais wa Shirikisho hilo katika Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO). 
(Picha zote na Benedict Liwenga)


Na Skolastika Tweneshe na Tupokigwe Marco. ­­
WAZEE wa shirikisho la filamu Tanzania (TAFF) hawajakubaliana na uamuzi wa Rais wa shirikisho hilo Bw. Simon Mwakifwamba kutogombea tena nafasi ya Urais katika shirikisho hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Msemaji wa wazee wa Shirikisho hilo Bw. Ahmed Olotu maarufu kama Mzee Chilo amesema kuwa wao kama Wazee wakongwe katika Shirikisho hilo wamemuomba Rais huyo agombee tena wadhifa huo kwa mara nyingine ili aweze kumalizia mambo muhimu ya maendeleo katika tasnia ya sanaa.

“Sisi kama wasanii na Wazee wakongwe katika tasnia hii, bila kushurutishwa na mtu yeyote tunapinga uamuzi wake wakutotaka kugombea tena nafafasi hiyo .” Alisema Olotu.

Aidha, ameongeza kuwa, miradi kama TAFF Trust Fund, TAFF Creative Ltd na mingine mingi yenye kuhitaji umakini ambayo imehasisiwa chini uongozi wake inahitajika kumaliziwa kwani bado haijakamilika.

Kwa upande wake Bi. Salome Nonge (Mama Abdul) ameeleza kuwa, Bwana Mwakifwamba ndiye aliyesaidia kupatikana kwa Ofisi ya Wasanii pamoja na usafiri katika kazi zao.

“Binadamu hakosi kasoro ila kwa Mwakifwamba ni ndogo mno sasa hatutaki mtu mwingine aje.”Bi Salome alisema.

Naye Bi. Salumu Ally (Mkasi) ameeleza kuwa uongozi wa Mwakifwamba umesaidia wasanii kupata haki zao kama hati miliki zilizowezesha kupata maendeleo ya kiuchumi kupitia sanaa wanaoifanya.


Hata hivyo sanaa ya filamu inakuwa kwa kasi nchini pamoja na changamoto zilizopo ambapo juhudi katika kutengeneza kazi zenye ubora zitakazoleta ushindani katika soko la kitaifa na kimataifa bado zinahitajika.

No comments: