Monday, December 14, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA VITUO VYA TELEVISHENI USIKU HUU

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, Mhe.William Lukuvi aagiza kupatiwa orodha ya wawekezaji kwenye ardhi nchini;https://youtu.be/DxnAMKWDltw

Waziri wa habari,utamaduni michezo na sanaa amewataka watumishi katika wizara hiyo kutimiza wajibu wao;https://youtu.be/E50hFInbZN8

Naibu waziri wa nchi ofisi ya Rais TAMISEMI, Mhe.Seleman Jaffo ametoa mwezi mmoja kwa halmshauri zote nchini kutumia njia ya TEHAMA kukusanya mapato; https://youtu.be/2on3XArsVuM

Bodi ya mkopo ya elimu ya juu imeagizwa kuwapatia  mikopo haraka wanafunzi  wanaostahili ; https://youtu.be/V5IOBeUNnYA

Wamiliki wa hoteli nchini wamehimizwa kujitokeza na kushiriki katika mpango wa mwaka mmoja wa mafunzo kazi kwa wanafunzi wa vyuo vya utalii nchini ili waweze kupata wafanyakazi bora;https://youtu.be/RIvi5icTUsc

Serikali ya awamu ya tano imesema inataka kuona sanaa inakuwa moja ya sekta muhimu katika kukuza uchumi wa msanii pamoja na taifa kwa ujumla; https://youtu.be/xJmNIs3d7pU

Mtu mmoja amefariki na wengine wanne kujeruhiwa katika mgogoro uliozuka baina ya wakulima na wafugaji mkoani Morogoro; https://youtu.be/7Vup8N-xeQA

Waziri wa ardhi nyumbana na maendeleo ya makazi Mh.Lukuvi amewaonywa wakekezaji wasioendeleza maeneo yao;https://youtu.be/mERDmyd4dnU

Mgombea ubunge jimbo la Arusha mjini kupitia CCM Philemon Mollel, amepinga ushindi alioupata mgombea wa CHADEMA, Godbless Lema; https://youtu.be/LLDbfi1Sgg8

Serikali imeliagiza jeshi la polisi mkoani Kilimanjaro kumkamata meneja wa kiwanda cha kukoboa kahawa cha Tanganyika kwa tuhuma za kuhusika kwa upotevu wa magunia 26;https://youtu.be/iKVVLlxdgLw

Shirika la maendeleo ya petrol TPDC limesema lina uwezo wa kukusanya taarifa za kitaalamu, zenye taarifa ya kilichopo chini ya ardhi; https://youtu.be/p8MnbzmvC2E

Shirika la umeme nchini TANESCO limetangaza kupata hasara ya shilingi milioni 200 kutokana na wizi wa umeme unaofanywa na baadhi ya wananchi hapa nchini; https://youtu.be/jkcA8EzCsN0

Waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezo Mhe.Nape Nnauye amesema atalishughulikia tatizo la udogo wa bajeti katika wizara yake; https://youtu.be/4S-QdTV8M3M

Siku chache baada ya bingwa wa zamani wa Olimpiki wa mbio za mita 800, Caster Semanya kufunga ndoa kimila mama yake amejikuta akiingia lawamani kumtetea mtoto wake;https://youtu.be/cJupE8ZAGyY

Waziri Sospeter Muhongo amesema upungufu wa umeme nchini unatokana na uchakavu wa mitambo na usimamizi mbaya wa matumizi ya maji. https://youtu.be/ampTSz9h9kg

Watanzania wametakiwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Magufuli katika kupambana na ufisadi kwani ni kikwazo kwa maendeleo ya taifa.https://youtu.be/rBlCxrV7Tms

Baada ya Rais John Magufuli kutangaza utolewaji wa elimu bure kuanzia mwakani, imeelezwa kuwa mwamko wa wazazi kuandikisha watoto umekuwa mkubwa sana. https://youtu.be/_DRh_RjFhxk

Mtu mmoja auwawa na askari 2 kujeruhiwa vibaya huku ngombe 70 wakiuwawa kufuatia mgogoro ulioibuka kati ya wakulima na wafugaji wilayani Mvomero. https://youtu.be/ov5HN-rrtjQ

Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi, awataka wakuu wa idara zote na watendaji wa wizara hiyo wakiwemo makamishina wa kanda kukutana DEC. 23 mwaka kupata taarifa ya matumizi fedha tangu july mwaka huu hadi hivi sasa.https://youtu.be/DrmWhdEXTLw

Mtu 1 auwawa na wengine 4 kujeruhiwa huku ngombe 70 wakiuwawa kufuatia mapigano kati wakulima na wafugaji wilayani Mvomero. http://simu.tv/XFi6VZM

Jeshi la polisi mkoani Mbeya limekamata shehena ya magogo 1613 aina Mninga yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 89.https://youtu.be/6bJnnmJWn3w

Rais John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Japan hapa nchini kuhusu masuala mbalimbali ya kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo ikulu jijini Dar es salaam.https://youtu.be/USDEUAm2vn0

Baada ya aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema kutetea kiti chake cha ubunge, Chama cha Mapinduzi CCM, chaazimia kupinga matokeo hayo mahakamani.https://youtu.be/bZSIilQpAbo

Katika tukio la aina yake watumishi na wahudumu wa klinik ya Foreplan pamoja na mmiliki wake Dkt.Mwaka wakimbia na kuwaacha wagonjwa wakiduwaa baada ya naibu waziri wa afya kufanya ziara ya kushitukiza kituoni hapo.https://youtu.be/PFzhn0SoZ68

Mamlaka ya mapato nchini TRA, yafanya ukaguzi kwa wafanyabiashara na taasisi mbalimbali zinazodaiwa kulimbikiza madeni kwa kutokulipa kodi. https://youtu.be/CT-Ip7JxpLs

Kamishina wa elimu nchini asema shule za msingi 11 za serikali hazitakuwemo kwenye mfumo wa utoaji wa elimu bure kufuatia shule hizo kuanzishwa kwa madhumuni maalum.https://youtu.be/KdCFC9dxczc

No comments: