Sunday, December 27, 2015

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI

SIMUTV:  Halmashauri ya jiji la Mwanza yapiga marufuku uuzaji vyakula katika maeneo yasiyo rasmi ili kuepukana na tishio la Kipindupindu.https://youtu.be/SkvwIPOtGxE

SIMUTV:  Wakazi zaidi ya 2800 wilayani Babati waiomba serikali kuchukua hatua za haraka kubatilisha maeneno ya shamba la Stella Estate na Krishina Seeds yaliyopo eneo lao ili kutoa nafasi kwa wananchi kufanya kilimo baada ya wawekezaji kushindwa kuyaendeleza kwa miaka 40.https://youtu.be/VR14JmpwAQg

SIMUTV:  Madereva wa malori na baathi ya wafanya biashara wa mahindi walalamikia ucheleweshaji wa kupakia mahindi katika kituo cha taifa cha kuhifadhia mahindi kanda ya Songea. https://youtu.be/3z4b5LgHaQM

SIMUTV:  Baadhi ya waganga wa tiba asili na tiba mbadala wagomea agizo la serikali la kutakiwa kuacha kujitangaza kwa madai ya kutoshirikishwa.https://youtu.be/WuWMIAgiawY

SIMUTV:  Viongozi wapya wa halmashauri ya mji wa Tunduma katika wilaya ya Momba jijini Mbeya waahidi kufanya mabadiliko makubwa katika miundombinu na mpangailio wa makazi ili mji huo uwe wa kisasa.https://youtu.be/dP-sOXa9-VE

SIMUTV:  Kamati kuu ya Chama cha mapinduzi CCM Zanzibar, yawataka wanachama wake kujiandaa na marudio ya uchaguzi visiwani humo.https://youtu.be/ZmOxZ8hyukk

SIMUTV:  Udogo wa kituo cha polisi cha wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara watajwa kuwa sababu kubwa ya polisi kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi huku miundombinu duni ikitajwa kuwa changamoto nyingine.https://youtu.be/bQtpIdZyLnY

SIMUTV:  Wakazi wa mikoa ya Shinyanga, Geita, Mwanza na Simiyu wajitokeza kuchangia damu kwa hiari ili kukabiliana na upungufu wa damu uliopo katika hospitali ya wilaya ya Geita hali inayosababisha vifo kwa kukosa huduma hiyo.https://youtu.be/em-z_TC6j14

SIMUTV:  Baadhi ya wakazi wa Wanging’ombe waiomba serikali kufanya uchunguzi wa mapato ya kijiji hicho pamoja na uharibifu wa mazingira unaofanywa na makapuni ya kutengeneza barabara.https://youtu.be/B0HmzxQiwVU

SIMUTV:  Kushuka kwa uchumi katika familia kwatajwa kuwa sababu kubwa ya wanamke wengi kuapata watoto nje ya ndoa jambo linalopelekea migogoro katika jamii. https://youtu.be/abCsRK2IhdY

SIMUTV:  Wakulima nchini watakiwa kutumia elimu mbalimbali wanazozipata kupitia mafunzo mbalimbali yanayotolewa na wataalamu wa sekta hiyo ili kuendesha kilimo chenye tija. https://youtu.be/Fyj2DXw11m0

SIMUTV:  Serikali mkoani Njombe imetumia Zaidi ya milioni 400 katika ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Wanging’ombe; https://youtu.be/D6mIiUJzepc

SIMUTV:  Serikali yapeleka huduma ya nishati ya mafuta wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ili kuboresha shughuli za uzalishaji; https://youtu.be/iJs5gwYFd1k

SIMUTV:  Wamiliki wa viwanda vya tumbaku mkoani Morogoro watakiwa kutenga asilimia kumi ya ajira kwa ajili ya vijana;https://youtu.be/2pSJQtbmTwg

SIMUTV:  Baadhi ya wazee mkoani Kigoma waiomba serikali kuhakikisha sera ya wazee ya mwaka 2003 inatungiwa sheria ili isaidie kutatua changamoto zinazowakabili wazee wengi hapa nchini; https://youtu.be/HwkloGQrb6c

SIMUTV:  Timu ya Azam imefanikiwa kuitungua timu ya Kagera Sugar ya mkoani Kagera kwa ushindi wa jumla ya magoli 2 kwa 0;https://youtu.be/0B3k0B6cH9k

SIMUTV:  Inaripotiwa kuwa mchezo wa kubashiri matokeo katika medani ya soka unazidi kushika kasi hapa nchini; https://youtu.be/hoCCpDLA3-8

SIMUTV:  Kukithiri kwa biashara haramu  ya ngono na tabia ya ushoga mkoani  Iringa kwadaiwa kusababishwa na wanafunzi wa vyuo vikuu:https://youtu.be/8RJjtZc2Aqo

SIMUTV:  Wakazi wa Mbeya vijijini wamedaiwa kuokoa takribani milioni 20 za serikali baada ya kuamua kuchangisha fedha na kujenga daraja kwa nguvu zao:https://youtu.be/6hXVffxaNR8

SIMUTV:  Waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa Dkt. Hussein Mwinyi amesema ukosefu wa ajira kwa vijana unatishia amani nchini:https://youtu.be/XncAYr3MMkc

SIMUTV:  Wakulima wa zao la mpunga mkoani Tabora wametakiwa kuachana na kilimo cha mazoea ili kuongeza uzalishaji wa zao hilo:https://youtu.be/8fti_HrnksI

SIMUTV:  Timu ya Simba yaendelea kudhoofishwa baada ya kutoka sare na timu ya Mwadui FC katika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga:https://youtu.be/fawKApidP3Y

No comments: