Tuesday, December 1, 2015

Masumin wadhamini midahalo ya wanafunzi wa sekondari Dar

Kampuni ya vifaa vya ofisi na mashuleni ya Masumin Printways na Five Star zimeamua kudhamini kwa muda wa miezi mitatu mdahalao wa kitaaluma kwa shule za sekondari za Dar es Salaam lengo likiwa kuongeza weledi wa wanafunzi katika masuala mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mdahalo uliohusisha Shule za Sekondari za St. Antony na Debrabant zote za Mbagala jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Masumin, Shakir Karim alisema kuwa wameamua kudhamini midahalo hiyo ili kuinua kiwango cha ufahamu kwa wanafunzi.

Alisema pia midahalo hiyo ambayo itakuwa kwa lugha ya kiingereza inatarajiwa kuwasaidia wanafunzi kuwa na uwezo mzuri wa kujieleza na kuchambua mambo kwa kutumia lugha hiyo ya kigeni ambayo imekuwa changamoto kubwa kwa walio wengi nchini.

“Tunathamini elimu na ndio maana kampuni yangu daima imekuwa ikijishughulisha na masuala ya vifaa vya shule na maofisini” alisema na kuongeza kuwa mpango wa sasa wa elimu bure utakuwa na manufaa kwa umma kwani kuna familia nyingi zilishindwa kusomesha kutokana na ada na michango mbalimbali.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi huo, mratibu wa midahalo hiyo, Shukuru Ngongoje alisema midahalo hiyo ambayo pia itaonyeshwa moja kwa moja na Kituo cha Luninga cha Channel Ten, itakuwa na msaada mkubwa kwa wanafunzi.

Alisema wameanza na shule hizo mbili na zingine zaidi zitaongezwa kulingana na makubalino baina yao na wamiliki wa shule ambao amewataka kumpa ushirikiano kwa faida ya wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam. 

Mwalimu wa taaluma katika shule ya Debrabant, Reginald Komino alisema siku za karibuni shule nyingi zimekuwa zikikwepa kuwapeleka wanafunzi wao katika midahalo hali ambayo kwa kiasi kikubwa inachangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini na uwezo wa wanafunzi kujieleza.

Alisema mratibu huyo kuwa siku za karibuni imekuwa shida kidogo kupata wanafunzi kwa ajili ya kushiriki midahalo ya kitaaluma ya namna hiyo na kizingizio kikubwa wanachotopa ni kuwa wapo katika program za shule zao za kuandaa kwa ajili ya mitihani hivyio hawana muda.

Alisema midahalo ina nafasi kubwa katika kuwajenga wanafunzi na kuwafanya wajiamini na kuwa na uwezo wa kujieleza mbele ya wenzao na pia inapanua ufahamu wao katikia masuala mbalimbali ambayo mengine si ya darasani.
Doreen Masau wa shule ya sekondari ya St. Antony akishiriki katika mdahalo wa kitaaluma ulioandaliwa na Masumon Printways na Five Star na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Mdahalo huo ambao ni kwa ajili ya shule za sekondaeri za Dar es Salaam uliihuisha pia shule ya Debrabant.
Sylivanus Ndayisenga wa shule ya sekondari ya Debrabant, akishiriki katika katika mdahalo wa kitaaluma ulioandaliwa na Masumon Printways na Five Star na kufanyika jijini Dar es Salaam jana. Mdahalo huo ambao ni kwa ajili ya shule za sekondari za Dar es Salaam uliihuisha pia St Antony.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Masumin Printways, Shakil Karim (kulia), akimkabidhi vifaa vya shule, Sylivanus Ndayisenga wa shule ya sekondari ya Sty Antony mara baada ya uzinduzi wa mdahalo wa kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam, juzi. Katikati ni mratibu wa mdahalo huo, Shukuru Ngongoje.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Masumin Printways, Shakil Karim (kulia), akimkabidhi vifaa vya shule, Doreen Masau wa shule ya sekondari ya St. Antony mara baada ya uzinduzi wa mdahalo wa kitaaluma kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Dar es Salaam, juzi. Katikati ni mratibu wa mdahalo huo, Shukuru Ngongoje. Picha na Mpigapicha Wetu.

No comments: