Friday, December 11, 2015

MADIWANI KUTOKA KATIKA MAJIMBO YA ILALA,UKONGA NA SEGEREA WAAPISHWA, UCHAGUZI WA KUMPATA MEYA NA NAIBU WAAHIRISHWA

Manispaa ya Ilala Dar es Salaam nako wameshindwa kuchagua Meya na Naibu Meya baada ya baadhi ya madiwani kuamua kukiuka taratibu za uchaguzi kwa kuamua kupiga picha kwa kutumia simu ya mkononi karatasi ya kupigia kura. 

Uchaguzi huo ulitakiwa kufanyika jana saa nne lakini kutokana na kuibuka kwa dosari hizo ambazo zilisababisha uchaguzi huo kuahirishwa.Baada ya kuahirishwa kwa uchaguzi huo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala ambaye alikuwa mwenyekiti wa uchaguzi John Ngonyani alisema wameamua kusitisha uchaguzi huo hadi kesho (leo), saa nane mchana kwasababu ya baadhi ya taratibu kukikuwa. 

Pia Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala Dar es Salaam Mashauri Mussimu alistoa ufafanuzi wa vipengele vya sheria ya uchaguzi huo ambapo alisema uchaguzi huo utakuwa wa siri kulingana na muongozo. 

Baada ya ufafanuzi huo, Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema), alisimama na kuomba muongozo ambapo alitaka uchaguzi huo uwe wa wazi na si kufanyika kwa siri. Madiwani wa Chadema wakati wanapiga kura hizo waliamua kuoneshana nani ambaye amepigiwa kura na hapo ndipo ilipoanza kuibua maswali miongoni mwa wajumbe wa uchaguzi huo. 

Wakati kwa madiwani wa CCM wao waliunga mkono mongozo wa kikao hicho kuwa kura iwe ni siri ya mpiga kura.Hata hivyo hakukua na maelewano na ndipo ilipoamriwa uchaguzi huo kuahirisha ambapo kabla ya uamuzi huo wasilitisha kikao kwa muda kwenda kupata muafaka lakini ikashindakana. 

Wapambe wa CUF na Chadema waliokuwa kwenye eneo hilo la ukumbi waliamua kuzomea madiwani wa CCM hasa kwa kuzingatia mbali ya kutakiwa kufanya uchaguzi wa meya na Naibu Meya kulifanyika tukio la kuapisha madiwani ambapo wengi wao walikuja na wafuasi wao.
SH1
Baadhi ya Madiwani kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea wakila kiapo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama Wilaya ya Ilala Mhe: Adelf Sachore (hayupo pichani) kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam (wakwanza kushoto), Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala Jimbo la Ukonga, Mhe: Tickey Kitundu (kulia katikati), Diwani wa Kata ya Kariakoo, Mhe: Abdulkarim Masaki.
PICHA ZOTE NA PHILEMON SOLOMON
SH2
Madiwani wakijaza fomu ya kiapo wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Viti Maalum Wilaya ya Ilala Jimbo la Ukonga, Mhe: Tickey Kitundu.
SH3
Madiwani wakijaza fomu ya kiapo.
SH4
Hakimu Mkazi wa Mahakama Wilaya ya Ilala Mhe: Adelf Sachore akiwaapisha Madiwani (hawapo pichani), kutoka katika Majimbo ya Ilala,Ukonga na Segerea kwenye Ukumbi wa Arnautoglo,Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.
SH5
Wageni waalikwa walioudhuria wakishuhudia Madiwani wakila kiapo.

No comments: