Mkurugenzi wa Mipango na Maendeleo ya Biashara, Mhandisi Kato Kabaka (aliyesimama), kutoka Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania akitoa elimu kwa wananchi wa kata ya Kisaki wilaya ya Morogoro Vijijini namna ya kutafiti nishati ya Jotoardhi hadi hatua ya kuzalisha umeme na jinsi itakavyoweza kubadili maisha ya wananchi wa kata hiyo.

Afisa Mawasiliano na Mahusiano ya Umma, Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania Bi. Johary Kachwamba, aliyesimama akiongea na wananchi wa kijiji cha Kichangani Morogoro Vijijini juu ya mikakati na mipango ambayo kampuni imejiwekea kuhakikisha megawati 200 za umeme zinalishwa nchini Tanzania kutokana na nishati ya Jotoardhi ifikapo mwaka 2020.
Mhandisi wa Mazingira wa Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi Tanzania Bi. Esther Range (aliyesimama) akiwaelimisha wananchi wa kijiji cha Kichangani namna ambavyo nishati ya umeme wa Jotoardhi ilivyo rafiki wa mazingira tofauti na nishati nyingine za umeme.
Mwananchi wa kijiji cha Kichangani Morogoro Vijijini Bwana Hamisi Kadobwa (aliyesimama) akiuliza swali kuhusu teknolojia ya kuvuna nishati ya Jotoardhi, aidha ilipongeza juhudi za Serikali kuwaletea wananchi maendeleo.
(Picha Na: Lilian Lundo – Maelezo)
No comments:
Post a Comment