Saturday, October 10, 2015

JUMUIYA YA MAAFISA AFYA ZANZIBAR YATOA MSAADA WA MAJI SAFI NA VIFAA TIBA, KAMBI YA WAGONJWA WA KIPINDUPINDU CHUMBUNI ZANZIBAR.

 Mratibu wa huduma za Afya ya Mama na Watoto Wilaya ya Magharibi Unguja Bi. Fatma Ussi Yahya (wa kwanza kulia) akitoa maelezo kwa wanajumuiya ya Maafisa afya Zanzibar walipotembelea kambi ya kipindupindu Chumbuni na kutoa msaada.
 Katibu wa Jumuiya ya Maafisa Afya Zanzibar Ahmed Suleiman akinawa mikono mara tu alipotoka  kwenye wodi za wagonjwa wa Kipindupindu.
 Picha ya pamoja ya wanajumuiya ya Maafisa Afya Zanzibar na wauguzi wa kambi ya Kipindupindu Chumbuni.
 Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maafisa Afya Zanzibar Salum Moh'd Abubakar akimkabidhi msaada wa maji Mratibu wa huduma za Afya ya Mama na Watoto Bi. Fatma Ussi Yahya kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa.
 Hapa akikabidhi boksi la gloves. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar.

No comments: