Thursday, September 3, 2015

WATANZANIA 500,000 WANATARAJIWA KUTEMBELEA HIFADHI ZA TAIFA

Mahmoud Ahmad Arusha
WATANZANIA 500,000 wanatarajiwa kutembelea mbuga zote 16 za hifadhi za taifa mwaka huu ikiwa ni hatua ya kuimarisha na kukuza utalii wa ndani ambapo watajionea vivutio mbalimbali vilivyomo ndani ya hifadhi hizo.

Hayo yameelezwa leo na Meneja uhusiano wa shirika la hifadhi za taifa, Tanapa, (Pichani)Pascol Shelutete, makao makuu ya TANAPA, jijini ,Arusha,  alipokuwa akizindua hatua ya mwisho ya  kampeni  maalumu ya miezi sita ya  kuhamasisha Watanzania kutembelea hifadhi  ili kujionea vivutio kwenye hifadhi wanazopakana nazo ili kuimarisha utalii wa ndani 

Kampeni hiyo ni Makakati maalumu uliobuniwa na Tanapa,  unaotoa  hamasa kwa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi zilizopo karibu na maeneo yao kwa gharama nafuu hasa siku za mwishoni mwa wiki na hivyo kuwapunguzia matumizi ya fedha wanazotumia kwenye starehe na badala yake wazitumie kutembelea hifadhi .

Meneja uhusiano wa Tanapa,  Shelutete, amesema kuwa  kadiri miaka inavyozidi kusonga mbele mwamko wa watanzania kutembelea mbuga za hifadhi unaongezeka, ambapo mwaka 2013 watanzania 362,217, walitembelea hifadhi zote 16 nchini, na mwaka 2014 watanzania 427,258 wametembelea mbuga hizo .

Amesema hatua ya mwisho ya uzinduzi wa kampeni hii inafanyika mkoani Arusha,ambao unapakana na mbuga za hifadhi za Arusha, Ziwa Manyara na Tarangire,na kampeni hiyo itadumu kwa muda wa miezi 6  na itahitimishwa Desemba mwaka huu.

Kauli mbinu ya kampeni hiyo ni “Tembelea hifadhi uzwadike , akatoa wito kwa watanzania kubadili mitizamo kwa siku za mwishoni mwa wiki zitumike kwa ajili ya kutembelea hifadhi badala ya kuzitumia kwa ajili ya starehe ambazo zinatumia fedha nyingi.

Uzinduzi huo umeshirikisha wakuu wa Idara za utalii wa hifadhi za Tarangire, Ziwa Manyara na hifadhi ya Arusha, pamoja na wadau ambao ni Chama cha waongoza utalii nchini TATO,ambao kwa pamoja wameelezea manufaa ya kutembelea hifadhi za taifa na sanjari kutatolewa zawadi mbalimbali kwa watanzania watakaotembelea hifadhi hizo.

1 comment:

Anonymous said...

Tanapa mnatakiwa kufanya jitihada za kuwafanya watanzania wengi watembelee vivutio vya utalii na sio kukaa kutangza kuwa mnatarajia watu kiasi kadhaa kuhudhuria.Hivi sasa hapa arusha mmewewka vijana na mabango wakionyesha mbuga zetu hili si jambo baya ila mwatakiwa kuandaa safari rahisi kwa watanzania kuwawezesha kutembelea mbuga zetu na kuona vivutio.