Monday, August 10, 2015

ZITTO ; FILIKUNJOMBE NI MCHAPAKAZI MZURI, CHIKU AMTAKA MBUNGE MSIGWA AONYESHE ALICHOFANYA JIMBONI

Ziito Kabwe  akiwa na mume  wa Chiku Abwao na Chiku Abwao  na kada wa ACT wazalendo.
Zitto kabwe  akiwa na wapambanaji
Zitto kabwe  akiwahutubia  wananchi wa jimbo la Iringa mjini
Chiku  Abwao  akiwahutubia wananchi wa jimbo la Iringa mjini
Mgombe  udiwani wa kata ya Mvinjeni Abuu Majeck akimpongeza mgombea  ubunge jimbo la Iri nga mjini Chiku Abwao.
KIONGOZI  wa  chama  cha ACT Wazalendo amempongeza mbunge wa  jimbo la  Ludewa  Deo Filikunjombe (CCM)  kuwa ni miongoni mwa wabunge wa mfano kutokana na utendaji kazi  wake mkubwa badala ya maneno bila  vitendo.

Huku aliyekuwa mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa na mjumbe wa kamati kuu ya Chadema Taifa  Chiku Abwao akimtaka  mbunge  wa  jimbo la  Iringa mjini Mchungaji  Peter  Msigwa (chadema) kuwaeleza  wakazi  wa jimbo  hilo ndani ya  miaka  mitano ya  ubunge  wake  amefanya  nini zaidi ya maandamano  na kutukana  watu .

Kauli   hiyo  waliotoa wakati  wa mkutano wa hadhara wa  kuwatambulisha   wagombea  ubunge  wa  jimbo la Iringa mjini na majimbo mengine ya  mkoa  wa Iringa na  kuwa siasa si maneno  matupu  siasa ni  kazi  zaidi ya  kuwakomboa wananchi   waliokuamini katika maendeleo .

Alisema  Bw  Kabwe  kuwa mbali ya  kuwa  yeye  ni  ACT  wazalendo  ila hata acha  kuwazungumzia  baadhi ya  wabunge   waliofanya kazi nzuri ya  kuwatumikia  wananchi  wao na  miongoni mwa  wabunge hao ni pamoja na mbunge wa Ludewa Bw Filikunjombe kwani kazi aliyoifanya  jimboni inaonekana na kazi aliyoifanya  ndani ya  bunge katika  kupigania maendeleo ya  wana Ludewa na  Taifa  kila mtazania anatambua mchango  wake .

Kwani  alisema  kuwa kati ya manho makubwa ambayo  Filikunjombe kama  makamu  wake  mwenyekiti  waKamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kamati liyoifanya  ni pamoja na  kuhakikisha ripoti ya Escrow inalindwa  pasipo  kuibiwa wakiwa wabunge  watatu ambao  walikesha  wakilinda  ripoti hiyo  isiibwe  na mawaziri  waliokuwa  wakizingira  jengo  walilokuwepo  ili  kuiba ripoti hiyo .

'' Siku   ile  tulikesha na mashuka  yetu ya  kimasai  kuhakikisha  ripoti yetu  haiibwi ili  tuiingize  bungeni  na tukaiingiza  bunge  lakini  ile  ripoti hadi  leo kuna  mambo hayajamalizwa  kwani kampuni ya IPTL ambao  imenunuliwa na kampuni ya PAP ya  Singa  singa na kampuni   hiyo ya PAP hadi leo bado inapokea Tsh  bilioni 4 kila mwezi kutoka  Tanesco  hapo  wazalishe ama  wasizalishe'' alisema  Kabwe


Alisema  kuwa kampuni  hiyo  asilimia 50  inamilikiwa na Seth Singa  singa na  asilimia 50  nyingine  zinamilikiwa na kampuni  inaitwa simba  Trust  iliyosajiliwa nje  ya  Tanzania  na  wamiliki  wake  hawafahamiki na  kuwa hizo ndizo  hoja ambazo  ACT wazalendo  wamejiandaa kutembea  nazo katika kampeni  ya uchaguzi mkuu .

Kabwe  alisema  kuwa sakata  ya ECROW  bado  halijaisha kwani  bunge liliagiza mtambo wa IPTL  utaifishwe  ila hadi  leo bado kuna  kigugumizi katika  kuchukua hatua  juu ya suala   hilo la kampuni ya kitapeli  kuendelea  kulipwa mabilioni ya shilingi  hivyo  alisema kuwa haja ya chama cha  kati  kuingia Ikulu ili  kuweza kupambana na mafisadi  wa Richimond ambao leo  wamejificha katika mwamvuli wa UKAWA .

Hivyo  alisema kuwa kila  sababu  wabunge kufanya kazi wanayotumwa na  wananchi  wao kwa uadilifu  badala ya  kuwa  wabunge wa maneno  bila  vitendo na kuwa wakati tukielekea katika  uchaguzi mkuu ni vema  wananchi  kuwapima  wabunge  wanaowachagua kwa  kueleza  wamefanya  nini majimboni  badala ya kuwa na mbunge  mpiga  kelele zisizo  za kimaendeleo kwa wananchi  wake .

Kwa  upande  wake  mgombea  ubunge  wa ACT wazalendo   jimbo la  Iringa mjini Bi Abwao  ambae  amejiunga na  chama  hicho kutoka Chadema  alisema mbunge  wa  jimbo  hilo mchungaji Msigwa ajiandae  kukabidhi  jimbo   hilo kwa  ACT wazalendo kwani ameshindwa  kuwatumikia  wananchi wa  jimbo la Iringa mjini kazi  waliyomtuma bungeni .

Alisema  kuwa kipindi  cha  miaka mitano ya  mbunge mchungaji Msigwa  jimboni hapo  hakuna  jipya ambalo amelifanya  zaidi ya  maandamano na  vurugu ambazo  wakazi  wa Iringa mjini hawajapata  kuziona na  kuwa atazunguka kila moja hadi nyingine  kuwaeleza  wananchi jinsi  ambavyo mbunge  huyo  alivyojaribu kuua nguvu  ya  vyama  vya  upinzani na  kushindwa  kuwajibika kwa wananchi  waliomchagua.

No comments: