Saturday, August 15, 2015

SIMU TV: HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI USIKU HUU

Watanzania wanaoishi nje ya nchi watakiwa kuacha woga wa kuwekeza nyumbani huku wakitakiwa  kuondokana na kasumba ya kwamba nyumbani kuna matatizo mengi. http://youtu.be/7fJnOQBNfyk

Wanafunzi wawili wapoteza maisha Mkoani Singida baada ya kugongwa na pikipiki muda mfupi baada ya kutoka darasanihttp://youtu.be/vi_iH8rPCDk

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA yakutana na wadau wa michezo lengo kujadili kwa pamoja sheria mpya ya ongezeko la dhamani inayolipwa na makocha na wachezaji. http://youtu.be/hwiKFJ4zMI8

Tanzania yabainika kua miongoni mwa nchi zinazotoa huduma bora ya usafiri wa anga ikiringanishwa na nchi nyingine za ukanda wa Afika Mashariki. http://youtu.be/CJCKT5av_Co

Zaidi ya wakazi 13,700 katika mikoa ya Pwani na Morogoro waanza kufaidika na miradi mipya ya maji iliyozinduliwa.http://youtu.be/YhD3DKopHTw

Kampuni ya Azam media yazindua rasmi huduma mpya ya Azam Sports HD itakayo onesha ligi kuu ya Hispania pamoja na michezo mbalimbali. http://youtu.be/vu3NCk65Dl4

Raisi Kikwete asaini hati za maadili kwa viongozi wa umma na sekta binafsi nchini leo hii jijini Dar es salaam. http://youtu.be/bsieNN--2G4

Raisi Jakaya Kikwete aongoza mamia ya wakazi wa Wilaya ya Mwanga katika mazishi ya aliyekuwa  Mwasisi wa Tanu na Asp Peter Kisumo. http://youtu.be/64_P7M_7pKI

CCM chakanusha taarifa zilizo sambazwa mitandaoni juu ya ahadi inayosemekana kutolewa na Dr.Magufuli kuwapa Laptop walimu wote nchini. http://youtu.be/5AcB8GGwHyY

Askofu mmoja wa kanisa la Tanzania Evangelism huko Shinyanga ahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la ubakaji.http://youtu.be/G3nf-I3XgUE

Uchimbaji wa gesi asilia Mkoani Mtwara walalamikiwa kupelekea uchafuzi wa mazingira kufuatia kuzagaa kwa tala ngumu.http://youtu.be/QTksCMn7QW4

Taasisi ya kuzua na kupambana na rushwa yawafikisha mahakamani afisa ugavi wa halimashauri ya jiji la Mwanza kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi. http://youtu.be/4c4l8ePGF5s

Wanawake wanao nyonyesha watakiwa kuzingatia lishe bora ili kuepukana na matatizo yanayoweza kuwapata watoto pindi wanapozaliwa. http://youtu.be/m_tyDgA1J3Y

Jeshi la wananchi watanzania JWTZ,lakanusha taarifa zilizo sambazwa na wanansiasa nchini juu ya kukusanya shahada za askari wakehttp://youtu.be/wVlbgIM6AVM

Bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini HESLB,yalia na wahitimu wasio rejesha mikopo kwenye bodi hiyo kwani wanawakosesha fursa wananfunzi wengine. http://youtu.be/Tz1WMrFQT2c

Wananfunzi wa shule ya msingi Maili moja iliyoko Pwani waiomba serikali kuwajengea madarasa kufuatia uhaba wa vyumba vya madarasa shuleni hapo. http://youtu.be/JqeZhDff1KA

Tume ya uchaguzi nchini NEC yasema wagombea wa urais na umakamu wanapaswa kurejesha fomu za kuwania nafasi hizo ifikapo agosti 21. http://youtu.be/xA9e-17byVY

CCM yasema kua kitendo cha wanachama wake kuhamia vyama pinzani hakiwatishi na sio mwanzo kwani viongozi wengi walioko vyama pinzani pia walitokea CCM. http://youtu.be/QheV8QhDpC8

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa azindua viwanja 5 vya michezo katika shule ya sekondari ya Nyamkumbu mkoani Geita. http://youtu.be/HeEJx8lLa1w

Benki ya NMB mkoani Iringa yakabidhi madawati 55 kwa shule ya sekondari ya Isimani iliyopo wilayani Iringa ikiwa ni sehemu ya madawati 163 yaliyotolewa na benki hiyo. http://youtu.be/GXya8Olye6o

Baadhi ya wanafunzi wa kike katika shule ya sekondari Selou iliyoko mkoani Ruvuma wakumbwa na ugonjwa usiofahamika wa kutikisa kichwa kisha kuanguka hovyo. http://youtu.be/b9xRkg6NAPU

Katika kuimarisha safu ya ulinzi katika klabu ya soka ya Simba washambuliaji 3 kutoka nchi za Burundi na Mali wasajiliwa kuiasaidia katika ligi kuu bara. https://youtu.be/63IrF7_iUk0

No comments: