Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi
(CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Njombe mjini
katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo katika
uwanja wa saba saba.Magufuli amesema akichaguliwa kuwa rais wa awamu ya
tano ataendeleza juhudi zake za kujenga barabara kwa kiwango cha
lami,amesema dhamira yake aliokuwa nayo ya Uwaziri wa Ujenzi katika
kujenga barabara za lami katika maeneo yote hapa nchini.
Amesema
tangu kupewa kuwa waziri wa ujenzi ameweza kujenga barabara zaidi
kilomita 7000 nchi nzima,ambapo ilipelekea kuongeza kuongeza pato la
mfuko wa barabara kutoka bilioni 73,3 hadi kufikia bilini 866 kwa mwaka
huu hivyo ameahidi akiwa rais atajenga zaidi barabara za lami.
Dkt
MAGUFULI ambae anaendelea na mikutano ya kampeni za Urais mikoa ya
nyanda za juu kusini , amelalamikia udanganyifu wa baadhi ya mitandao ya
kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuripoti kuwa amelazwa wodi ya
wagonjwa mahututi katika hospitali ya mkoa wa mbeya wakati sio kweli.
Aidha pia Magufuli amewaomba wananchi waweke imani kubwa kwake kwa kumpa kura nyingi zitakazomwezesha
kuwa raisi wa awamu ya tano,na kIsha alipe fadhira hizo kwa kutatua
kero zinazowakabili hasa wananchi wenye kipato cha chini
Mgombea
Urais wa CCM Dkt Joh Pombe Magufuli akipeana mkono na Makamu Mwenyekiti
wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula mara baada ya kumkaribisha
mgombea huyo jukwaani kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za
chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha
awamu ya tano
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Ndugu Phillip Mangula akiwashukuru
wananchi wa Njombe waliojitokeza kwa wingi kwenye mkutano wa hadhara wa
kampeni,uliofanyika jioni ya leo katika uwanja wa sabasaba mjini
humo,ambapo pia Ndugu Mangula alimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt
John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi wa njombe na kuzinadi sera za
chama chake na kuomba ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika kipindi cha
awamu ya tano
Wananchi
wa Njombe wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Magufuli kwenye
mkutano wa kampeni uliofanyika jioni ya leo kwenye uwanja wa sabasaba
mjini Njombe.
Mjumbe
wa Halmashauri kuu ya CCM na Mgombea Ubunge wa jimbo la Kyela,Mh
Harrison Mwakyembe akiwahutubia wananchi wa Njombe jioni ya leo kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni
Waanchi wakishangilia jambo kwenyemkutano wa kampeni wa CCM.
Mgombea
Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa jimbo
la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga ndani ya wilaya
hiyo ya Wanging'ombe
Mgombea
Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM mgombea
Ubunge wa jimbo la Wanging'ombe Mh. Gerson Lwenge kwa wananchi wa Makoga
ndani ya wilaya hiyo ya Wanging'ombe kwa ajili ya kuwaambia wananchi ni
namna gani wataiongoza Tanzania katika awamu ya tano.
Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge wa
jimbo la Makete Dkt Norman Msigala kwa wananchi wa Makoga ndani ya
wilaya hiyo ya Wanging'ombe
MKutano wa Kampeni ukiendelea.
Wananchi
wakisikiliza sera za mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe
Magufuli,hayupo pichani alipowahutubia jioni ya leo mjini Njombe.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa hadhara wa kampeni
Wananchi
wakiwa na mabango yao ya kumsifu na kumkaribisha mgombea Urais wa CCM
Ndugu John Pombe Magufuli,mara baada ya kufunga barabara alipokuwa
akipita katika kijiji cha Mgagala akielekea mkoani Njombe kwenye mkutano
wa kampeni
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Makoga katika wilaya ya Wanging'ombe mapema leo mchana.
Wananchi wa kijiji cha Ikonda wakimsikiliza Dkt Magufuli
Bango
No comments:
Post a Comment