Wednesday, July 8, 2015

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAENDELEA KUMWAGA ELIMU KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2015

Mtaalam kutoka Kituo cha Jimolojia Tanzania (TGC), Jumanne Shimba (kulia) akielezea shughuli za kituo hicho kwenye banda la Wizara ya Nishati na Madini.
Mtaalam katika Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Rayson Nkya (kushoto) akielezea sera ya madini kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mtaalam kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Ayoub Shija akielezea shughuli za mgodi huo katika banda la Wizara ya Nishati na Madini.
Mtaalam kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) Steven Lowoko akitoa maelezo juu ya jinsi mtambo wa kufua umeme kwa kutumia maji unavyofanya kazi kwa kutumia mfano wa mtambo huo kwa baadhi ya wanafunzi waliotembelea banda la TANESCO.
Afisa Mawasiliano kutoka Mpango wa Kuongeza Uwazi na Uwajibikaji katika Tasnia ya Uziduaji Nchini (TEITI), Godwin Masabala akitoa maelezo jinsi taarifa za mapato yatokanayo na rasilimali za gesi na madini zinavyokusanywa.
Afisa Huduma kwa Wateja katika Shirika la Umeme Nchini(TANESCO), Lucas Kusare (katikati) akielezea shughuli za shirika hilo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Tanesco.
Afisa Uokoaji katika Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Evarist Mwanakatwe (kulia) akielezea shughuli za uokoaji zinavyofanyika katika mgodi huo pindi majanga yanapojitokeza.
Baadhi ya wananchi wakiangalia aina mbalimbali za madini katika banda la Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST).
Mtalaam kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), Kankila Wakimbili akielezea shughuli za wakala huo kwa wananchi waliotembelea banda hilo.
Mtaalam katika Chuo cha Madini Dodoma(MRI), Mkunde Msaky (kulia) akielezea fani zinazotolewa na chuo hicho kwa wananchi waliotembela banda hilo.
Wataalam katika Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST) wakiwa katika picha ya pamoja.

No comments: