Tuesday, July 28, 2015

Wizara ya Habari na ESAMI yawapiga msasa Maafisa Vijana

Maafisa Vijana Nchini wametakiwa kutumia elimu wanayopata katika kuwaendeleza vijana kiuchumi ili kuwawezesha kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali. 

Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa awamu ya kwanza ya mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu.

Bw. Kajugusi alisema kuwa kwa kutambua umuhimu wa kuwaendeleza vijana nchini Wizara kwa Kushirikiana na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) wameanzisha mradi unaolenga kuwawezesha vijana kijasiriamali nakiubunifu kwa kupitia mafunzo wanayowapa Maafisa Vijana.

“tunawaomba kushiriki kikamilifu katika mafunzo haya ya ujasiriamali na ubunifu kwa kuwasikiliza wawezeshaji kwa makini kwa dhumuni la kutumia elimu hiyo kuwainua vijana nchini kiuchumi na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika ujasiriamali”. Alisema Kajugusi.

Naye Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Bw. Leon Malisa alisema kuwa dhumuni la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Maafisa Vijana katika eneo la  ujasiriamali na ubunifu ili kuwawezesha kuitumia Elimu hiyo kwa vijana vijana nchini kwa kuwawezesha kujiajiri wenyewe.

Aidha Bw. Malisa ametaka vijana nchini kuunda vikundi na kubuni miradi itakayowaendeleza ili Wizara kwa kushirikiana na ESAMI waweze kuwasaidia kujiendeleza ikiwa ni njia moja wapo ya kukabiliana na tatizo la Ajira Nchini.

Akizungumzia kuhusu mafunzo hayo Afisa Vijana toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliackim Mtawa alisema kuwa watatumia mafunzo haya kuwatayarisha vijana kuwa wajasiriamali wazuri na kuwasimamia katika utekelezaji wa Miradi hiyo ili kuwawezesha kushiriki katika uzalishaji mali na kukuza uchumi kupitia ujasiriamali.

Mafuzno hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI)
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi akiongea na Maafisa Vijana waliohudhuria Mfunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu kutumia elimu na uzoefu watakaoupata katika mafunzo hayo kuwainua vijana kiuchumi kwa kutoa elimu itakayowajenga na kuwafanya vijana kujitegemea na kuwa wajasiriamali, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha. Kulia ni Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon Malisa.
Baadhi ya Maafisa Vijana wakimsikiliza Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. James Kajugusi wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo hayo.
Mkurugenzi wa Ujasiriamali na Ubunifu kutoka Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) Bw. Leon Malisa akiongea na Maafisa Vijana na kuwataka kushiriki kikamilifu katika mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yanayotolewa kwa ushirikiano wa Chuo hicho na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ili kuweza kuendeleza na kukuza ujasiriamali hasa kwa Vijana, wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo leo Jijini Arusha.
Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa akiwaeleza jambo Maafisa Vijana, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute)leo Jijini Arusha.
Muwezeshaji Prof Bandali Batchu akiwasilisha Mada wakati wa Mafunzo hayo leo Jijini Arusha.
Prof Bandali Batchu Akiwaeleza jambo Maafisa Vijana wakati wakiwasilisha mada katika mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute) leo Jijini Arusha.
Baadhi ya Maafisa Vijana wakiwa katika mijadala wakati wa mafunzo ya Ujasiriamali na Ubunifu yaliyoandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha ESAMI (Eastern and Southern Africa Management Institute)leo Jijini Arusha. PICHA NA HASSAN SILAYO-MAELEZO

No comments: