Saturday, July 25, 2015

TTCL yaunganisha Ofisi na Kanda za MSD kwenye Mkongo

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) hati ya makubaliano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania. Hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) hati ya makubaliano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania. Hafla hiyo ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.  Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akizungumza katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania inayotolewa na kampuni ya TTCL. Ofisi za Kanda za MSD zimeunganishwa na Makao Makuu na huduma za mkongo wa mawasiliano ili kufanya kazi zake kwa haraka na ufanisi zaidi.Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia. Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (kushoto) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD) leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD Dar es Salaam, kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota akishuhudia.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (kulia) akisaini hati ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania (MSD), kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani akishuhudia kabla ya kukabidhiwa.Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa nne kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL. Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Peter Ngota (wa tatu kulia) na Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani (wa nne kushoto waliokaa) katika picha ya pamoja na baadhi ya maofisa wa kampuni ya Simu Tanzania na Bohari ya Dawa Nchini katika hafla ya makabidhiano ya mradi wa huduma za mkongo kwa ofisi za Bohari ya Dawa Tanzania na kampuni ya TTCL.

 KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imekabidhi mradi mkubwa wa Mkongo wa Mawasiliano ambao umeyaunganisha matawi yote ya Bohari ya Dawa Nchini (MSD) na Makao Makuu ili kufanya kazi zake kwa haraka na kwa ufanisi. Hafla ya kukabidhi mradi huo imefanyika leo Makao Makuu ya Ofisi za MSD zilizopo jijini Dar es Salaam. 

 Akikabidhi mradi huo, kwa niaba ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura, Ofisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Simu Tanzania, Peter Ngota alisema kampuni hiyo inajisikia fahari kufanikiwa kuunganisha ofisi zote za kanda za MSD na Makao makuu kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ni salama na wauhakika katika utendaji wa kazi. 

 Alisema MSD ni moja ya wateja wake wakubwa ambao wameunganishwa kihuduma kupitia mkongo wa mawasiliano ambao ufanisi wake ni mkubwa na salama kwa wateja tofauti na teknolojia nyingine za mawasiliano. Alisema huduma za mkongo wa mawasiliano zinazotolewa na TTCL kwa wateja wake ni salama na zenye ubora katika ufanisi jambo ambalo limevuta idadi kubwa ya wateja kuongezeka kila uchao. 

 Alisema kwa sasa TTCL inatoa huduma hizo kwa makampuni ya simu, taasisi mbalimbali za umma na binafsi, mabenki, hospitali kadhaa, vyombo vya habari, wateja binafsi pamoja na mataifa kama Rwanda, Burundi, Uganda, Kenya, Zambia na nchi ya Malawi. 

 Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa mradi huo, Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Cosmas Mwaifwani alisema MSD ilianza kufungiwa mawasiliano ya mkongo Mwezi Mei, 2011 kwa kuunganisha ofisi za makao makuu na baadaye ofisi mpya za mauzo zilizopo Muleba zilizounganishwa mwaka 2013. 

 Alisema MSD ilifanya uamuzi wa kuhamia kwenye teknolojia ya Mkongo baada ya kuona uwepo wa matatizo makubwa yaliyokuwepo katika teknolojia ya awali ambayo ni waya wa jadi yaani shaba ambayo pia ilitolewa na kampuni ya TTCL. 

 "...Bohari ya Dawa iliamua kuhamia katika teknolojia hii baada ya kufanya utafiti wa kina na kuona faida ambazo zinaweza kupatikana kwa kutumia teknolojia hii (mkongo) na hivyo kuachana na matatizo yanayosababishwa na teknolojia ya shaba. Hii ina maana mkongo unaweza kubeba habari zaidi na kwa ubora mkubwa kuliko waya wa shaba," alisema Mwaifwani. 

 Alisema kwa sasa MSD imeanza kupata mafanikio makubwa baada ya kuanza kutumia huduma za mkongo na tayari TTCL imeyaunganisha Ofisi 10 za MSD ambazo ni Kanda nane (8) pamoja na vituo viwili vya mauzo; alizitaja Kanda zilizounganishwa ni pamoja na Dar es Salaam, Moshi, Iringa, Mbeya, Mwanza, Tabora, Dodoma, Mtwara, Muleba, Tanga, Makao Makuu ya Muda Jamana na Ofisi za Keko Mwanga. 

 "...Tunasema kwamba Bohari ya Dawa imedhamiria kuokoa maisha ya Watanzania kwa kutumia teknolojia ya Mkongo yenye kasi zaidi, usalama, na gharama nafuu zaidi katika kuhakikisha dawa zenye ubora zinamfikia kila Mtanzania kwa wakati na kupunguza kero ya kusubiri huduma zetu kwa muda mrefu kwani sasa huduma zinapatikana kwa wakati kwa kuwa teknolojia inayotumika ni ya kisasa na yenye ubora wenye kukidhi viwango vinavyohitajika na bohari ya dawa," alisema Mkurugenzi Mkuu, Mwaifwani.

No comments: