Wednesday, July 29, 2015

MAMA SALMA KIKWETE ATEMBELEA HOSPITALI YA CANIBERRA NCHINI AUSTRALIA

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa na Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Caniberra nchini Australia inayotoa huduma ya Afya ya Mama, vijana na watoto mara baada ya kufika eneo la hospitali kwa madhumuni ya kujionea namna bora yautoaji huduma. Mama Salma yupo nchini Australia akifuatana na mumewe Rais Jakaya Kikwete kwenye ziara rasmi ya kiserikali nchni humo.
Mke wa Rais na Mama Salma Kikwete na mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CaniberraMama Elizabeth Chatham wakibadilishana mawazo wakati walipokuwa wakitembelea maeneo mbalimbali ya kutolea huduma ya mama, vijana na watoto.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwaangalia baadhi ya watoto wanapatiwa huduma ya matibabu katika hospitali ya Caniberra wakijishughulisha na michezo mbalimbali wakiwa na wazazi wao.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimpa pole na kumtakia apone haraka binti Addison Stephen,6, aliyevunjika mguu na kufungwa PoP na hatimaye kulazwa hospitalini hapo huku akihudumiwa na baba yake Mzazi Bwana Stephen Miles (aliyesimama kulia) na aliyechuchumaa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo Mama Elizabeth Chatham.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimbeba mtoto mchanga Isabella mwenye umri wa siku moja aliyezaliwa na uzito wa kilo 3 na gramu 8 katika hospitali ya Caniberra nchini Australia huku wazazi wake Bwana Steven Fanner,34, na Bibi Tania Mras,32, wakishuhudia tarehe 28.7.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake,WAMA, Mama Salma Kikwete akimkabidhi jarida linalochapishwa na Taasisi yake kwa Mama Elizabeth Chatham, Mkurugenzi Matendaji wa Hospitali ya wanawake, vijana na watoto ya Caniberra nchini Australia mara baada ya kutembelea sehemu mbalimbaali za kutolea huduma hospitalini hapo yarehe 28.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Gavana Jenerali wa Australia Mama Cosgrove mara baada ya Rais Kikwete kukutana na Gavana Generali wa nchi hiyo Mheshimiwa Peter Cosgrove kwenye Ikulu ya nchi hiyo tarehe 28.7.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitia saini kitabu cha wageni kwenye Ikulu ya Australia huku Rais Dkt. Jakaya Kikwete na Mwenyeji wake Gavana Jenerali Peter Cosgrove na Mkewe wakishuhudia. PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments: