Tuesday, July 7, 2015

HABARI TOKA VITUO MBALIMBALI VYA TELEVISHENI

CH10 NEWS
Umoja wa Vyama vya umoja wa katiba ya wananchi UKAWA, wamshauri raisi Kikwete kuto saini miswada ya mafuta na gesi kwa maslahi ya taifa. http://youtu.be/b0cf6mJxYJA
 Waziri wa mambo ya ndani Mathias Chikawe, asema usalama wa nchi ndani na mipaka ni madhubuti na wananchi waendelee na ujenzi wa taifa. http://youtu.be/1NhCGk7W5nc
Kiwango cha maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi kimeshuka kwa kiasi kikubwa kufuatia juhudi za serikali na baadhi ya taasisi katika kutoa elimu dhidi ya ugonjwa huo. http://youtu.be/NdwvPa9tvjk
 Tume ya uchaguzi ya Zanzibar ZEC, yataja majimbo mapya ya uchaguzi na kubadili mipaka iliyokuwepo awali. http://youtu.be/rs9-FmUO5Zg
 Serikali yapiga marufuku makundi ya wapambe wa wagombea yaliyoandaliwa kuelekea Dodoma kushuhudia uteuzi wa wagombea wao huku hatua kali zikitolewa dhidi yao. http://youtu.be/Eu8gqh4Ex28

TBC NEWS
 Spika wa Bunge Anne Makinda aishauri serikali kujenga mfumo imara wa nidhamu katika usimamizi na matumizi ya fedha za gesi nchini. http://youtu.be/M5HzjhxvEIc
 Jeshi la polisi mkoani Tabora laendesha operesheni maalum kukamata watu waliovamia msitu wa igombe na kufanya uharibifu mkubwa na kuhatarisha Bwawa la Igombe. http://youtu.be/-WWqSJRFqTI
 Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wausogeza mbele uchaguzi wa wabunge na uraisi ili kuweza kupata muda wa kuujadili uchaguzi huo. http://youtu.be/5nW8okoqIQ8
 Makamo wa pili wa Raisi Dr.Bilal asema utumiaji wa mbegu bora nchini na Afrika kwa ujumla si mzuri kutokana na kutumia kiwango kidogo cha mbegu zilizo zalishwa katika vituo vya utafiti. http://youtu.be/0BaV8jjwhE4
 Jaji mkuu wa Tanzania Othman Chande asema  idara ya mahakama inazidi kuboresha huduma zake ilikuwa karibu zaidi na wananchi. https://youtu.be/PZKbXlABi1U

STAR TV NEWS
Kufuatia adhabu iliyotolewa kwa wabunge wa upinzani, wabunge wote wa UKAWA waadhimia kutohudhuria vikao vyote vilivyobakia. http://youtu.be/cMNq8IW44vk
 Jeshi la polisi Mkoani Morogoro linawashikilia watu 2 kwa kukutwa na silaha aina ya shot-gun wakiwa katika maandalizi ya kufanya uhalifu. http://youtu.be/O0eIBivlMQM
 Wakati siku za kuelekea uchaguzi mkuu zikiyoyoma, mgombea uraisi na mhadhiri Mchungaji Malisa abadili azimio lake la awali na kuhaidi kugombea kupitia chama cha CCK. http://youtu.be/a0IKvinUQ1U
 Wizara ya mambo ya ndani imefanikiwa kuwafuta kazi askari polisi 70 na askari uhamiaji 21 baada ya kubainika kujihusisha na vitendo vya rushwa katika awamu ya 4. http://youtu.be/VJDdJZd2xLA

 AZAM TV NEWS
Raisi Nkurunzinza wa Burundi asusia kikao maalum cha wakuu wa EAC jijini Dar es salaam huku akiwakilishwa na waziri wake.http://youtu.be/jabCkjKdFXg

Wakulima wa zao la korosho hapa chini waeleza kukumbwa na changamoto kubwa inayowafanya washindwe kushindana kimataifa. http://youtu.be/jK8gglVO4Uo
 Jamii ya watu wenye ulemavu yashauriwa kuachana na fikra za utegemezi kutokana na hali walizo nazo jambo ambalo linawafanya wajikute wakiwa ombaomba. http://youtu.be/GtXRPXxz9K8
 Msanii wa nyombo za Taarabu, Mzee Yusuph atangaza nia ya kuwania ubunge  huko Zanzibar. http://youtu.be/4Eh442-J89E
 Zoezi la uandikishaji BVR visiwani Zanzibar limekalima mwishoni mwa wiki huku vyama vikuu vya upinzani vikilalamikia jinsi zoezi hilo lilivyo endeshwa. http://youtu.be/onTj6UuK_Vw

No comments: