Wednesday, July 1, 2015

Airtel Fursa Yatumia zaidi ya milioni 3 kumpiga tafu mjasiliamali mwingine - Airtel Fursa wiki hii kuwafaidisha mamia ya vijana Mwanza

Mariam Mrisho akifungua jokofu
baada ya kukabidhiwa.
AIRTEL Tanzania kwa kupitia mpango wake kusaidia jamii wa Airtel Fursa“Tunakuwezesha” imemkabidhi jokofu na vifaa mbalimbali, Mariam Mrisho (23) vyote vyenye thamani ya milioni 3 ili vimsaidie katika katika biashara yake ya kutengeneza vyakula ‘mama lishe’ na kumuongezea uzalishaji na kipato chake kwa ujumla.
Mariam Mrisho ni kijana mwingine wa kitanzania kati ya wengi waliofaidika na Airtel Fursa hivi karibuni kwa kuingia  kwenye historia ya kusaidiwa kwa kupatiwa misaada na wengine kuwezeshwa kwa kuhudhuria warsha za Airtel Fursa kwa lengo la kuwawezesha vijana hao wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24 kutimiza ndoto zao kikamilifu kwa kuwafundisha jinsi ya kupambana na changamoto zinazowakumba.
Akizungumza baada ya makabidhiano, Meneja Huduma kwa Jamii wa Airtel Tanzania, Hawa Bayumi alisema “Airtel Fursa  tunaamini tukiwezesha vijana nchini na wao ni wataweza kuchangia jamii nzima, vijana wananafasi kubwa sana kwenye jamii. Hatuishii hapa bali mwishoni mwa wiki tutakuwa Mwanza ‘Rock City’ ambapo pia tutakutana na mamia ya vijana na tutafanya warsha itayofundisha vijana wetu mambo mengi ikiwemo jinsi yakupata na kusimamia mtaji, masoko, namna ya kuendesha biashara au jinsi ya kuzitambua fursa pale waliko”.
“Vijana wa Mwanza jitokezeni kwa wingi jumamosi hii tarehe 4, tutakuwa pale ukumbi wa halmashauri ya jiji Mwanza mjini ili tukuwezeshe kwa kugawana ujuzi toka Airtel Fursa kama tulivyomuwezesha Mariam Mrisho wa Dar” alisisitiza Bayumi.
Kwa upande wake Mariam ambaye anategemewa na familia yake alieleza kuwa alikuwa akifanya kazi ya kuajiriwa kwa mama lishe lakini kutokana na kuthubutu na jitihada zake aliaamua kuacha na kuanzisha biashara yake ya kuuza vitafunwa na ndipo akasikia habari za Airtel FURSA na akaamua kuainisha changamoto zake na kuzituma ili kuingia katika mpango  huo.

“Nilishajitoa kufanya shughuli za mama lishe nikiwa nimeajiriwa baada ya hapo nikaamua kuingia katika shughuli zangu mwenyewe na nikajikita zaidi katika kuuza vitafunwa, nilijitahidi sana kudamka alfajiri ili kufikia malengo yangu ya mimi pia kusaidia jamii yangu lakini nikajikuta napambana na changamoto za ukosefu wa vifaa hivi vyote, kwa kweli iliniwia ngumu kwa kiasi fulani lakini leo nawashukuru sana Airtel Fursa wameniona baada ya mimi kuandika maombi yangu  kwao”. Alieleza Mariam
Kwa kweli nitafanya kazi kikamilifu ili niwe balozi bora na baadae niweze kusaidia hata wenzangu wenye mahitaji kama yangu” alisisitiza Mariam
Bayumi pia aliwataka vijana toka mikoa yote ya kanda ya ziwa kufika kwa wingi ili wakutane na wataalam wa Airtel Fursa huku akielekeza kuwa bado Airtel Fursa inapokea maombi ya vijana wanaotamani kusaidiwa toka mahali popote katika namba yao ya sms ya 15626 au wanaondika barua pepe kwenda airtelfursa@tz.airtel.com   kwa kuandika jina, umri, mahali anapoishi pamoja na aina ya biashra wanayofanya ili kuweza kupitiwa na kuwezeshwa na Airtel.

No comments: