Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwapungia mikono wafuasi wake waliofika katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee hiyo(Habari picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli,Edward Lowasa akiwa sheikh mkuu wa Bakwata mkoani Arusha,Shaaban Juma wakifurahia jambo katika hafla ya harambe ya ujenzi wa msikiti wa Patandi iliyofanyika jana katika uwanja wa msikiti mkuu wa mkoa Arusha,jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana.
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa akiwa anasalimiana na baadhi ya wadau waliokuja kumuunga mkono katika uwanja wa msikiti mkuu katika hafla ya harambee ya ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo jumla ya kiasi cha zaidi ya sh,200 milioni zilipatikana katika harambee
Msafara wa pikipiki
Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa jimbo la Monduli mkoani Arusha,Edward Lowasa anatarajia kutangaza nia ya kuwania nafasi ya Urais kupitia CCM mnamo Mei 24 mwaka huu katika uwanja wa michezo wa Sheikh Amri Abeid uliopo jijini Arusha.
Lowasa,alitoa kauli hiyo leo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti wa Patandi ambapo alifanikisha kuchangisha jumla ya zaidi ya kiasi cha sh,200 milioni ambapo watu mbalimbali walimuunga mkono katika harambee hiyo.
Akizungumza katika hafla hiyo leo kwa mafumbo Lowasa alisema kuwa mnamo Mei 24 mwaka huu anataraji kusema neno ambalo atahitaji wananchi wamuunge mkono siku hiyo.
"Niseme neno nisiseme,tarehe 24 mwezi huu katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid siku hiyo nitasema neno ambalo nitahitaji mniunge mkono ambalo nitahitaji mniunge mkono "alisema Lowasa
Lowasa kwa kujiamini aliwaomba kila mkazi wa Arusha siku hiyo kutoka na kuja uwanja huo na kumuunga mkono katika safari yake ya matumaini.
"Ukiulizwa unaenda wapi sema unakuja kuniunga mkono katika safari yangu ya matumaini"alisisitiza Lowasa
Hatahivyo,Lowasa aliipongeza kamati ya amani ya mkoa wa Arusha inayoundwa chini ya Askofu wa kanisa katoliki la jimbo kuu mkoani Arusha,Josephat lobullu kusimamia amani ya mkoa huo.
Aliipongeza kamati hiyo na kusema kuwa amani ya mkoa wa Arusha ni muhimu kuliko jambo lolote kwa kuwa Arusha ni mji ambo ni chanzo cha utalii duniani.
"Tuendelee kuheshimiana bila kujali misingi ya dini,kabila au rangi lakini niipongeze kamati ya amani ya hapa Arusha kwa kuwa Arusha ni mji wa kitalii bila amani hakuna utalii Arusha"alisema Lowasa na kuibua shangwe
No comments:
Post a Comment