Saturday, April 18, 2015

MKUU WA WILAYA YA TEMEKE NDUGU SOPHIA MJEMA AFUNGA RASMI MAFUNZO YA SIKU 5 YA KUZUIA MIMBA ZA UTOTONI KWA WANAFUNZI WA SEKONDARI WILAYANI TEMEKE

Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akilakiwa na Dkt. Martha Kisanga, Meneja wa Kanda ya Pwani wa Shirika la Engender Health mara baada ya kuwasili kwenye eneo la Shule ya Sekondari Kibasila kwa ajili ya kufunga rasmi mafunzo ya siku 5 yaliyohusu mradi wa kuzuia mimba za utotoni katika Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke tarehe 17.4.2015. Waliosimama katikati ni Ndugu Donald Siliva, Afisa-Elimu Sekondari, Wilaya ya Temeke na Dkt. Sarah Maongezi, Mkurugenzi wa Afya kutoka Taasisi ya WAMA.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akisalimiana na baadhi ya wanafunzi kutoka baadhi ya Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke walioshiriki katika mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni. Mafunzo hayo yalifanywa na Taasisi ya WAMA ikishirikiana na Shirika la Engender Health kwa ufadhili wa Shirika la Misaada la Marekani, USAID.
Baadhi ya wanafunzi na walimu kutoka Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakiimba wimbo wa kumkaribisha mgeni rasmi alipokuwa akiingia ukumbini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kutoka Wilaya ya Temeke wakimsikiliza salamu kutoka Taasisi ya WAMA zilizotolewa na Meneja wa Uragibishi na Mawasiliano wa Taasisi ya hiyo Ndugu Philomena Marijani wakati wa sherehe ya kufunga rasmi mafunzo hayo huko Kibasila Sekondari tarehe 17.5.2015.
Meneja wa Uragibishi na Mawasiliano kutoka Taasisi ya Wana wake na Maendeleo, Ndugu Philomena Marijani akitoa maelezo ya awali kuhusiana semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke iliyofanyika huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.



Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akitoa hotuba ya kufunga rasmi mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari za Wilaya ya Temeke yaliyofanyika Kibasila Sekondari.
Washiriki wa semina ya siku 5 ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Shule za Sekondari katika Wilaya ya Temeke wakifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni rasmi wakati akifunga rasmi mafunzo hayo huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Ndugu Sophia Mjema akiwaaga washiriki wa mafunzo ya kuzuia mimba za utotoni kwa wanafunzi wa Sekondari katika Wilaya ya Temeke huko Kibasila Sekondari tarehe 17.4.2015. PICHA NA JOHN LUKUWI

No comments: