Wednesday, March 18, 2015

MFANYABIASHARA MASHUHURI MIKOA YA ARUSHA NA KILIMANJARO VICENT LASWAI APANDA MLIMA KILIMANJARO

Mfanyabiashara mashuhuri katika mikoa ya Arusha na Kilimanjaro,Vicent Laswai akitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika ofsi za Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA) kabla ya kuanza safari ya kupanda Mlima Kilimanjaro.
Mfanyabiashara Vicent Laswai akijadiliana jambo na Mhifadhi mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro(KINAPA) ,Erastus Rufungulo kabla ya kuaza safari ya kupanda mlima Kilimanjaro. kulia ni mkurugenzi wa kampuni ya Topi Raisen Richard Mardai 
Mfanyabiashara Vicent Laswai akiwa na Mhifadhi mkuu KINAPA ,Erastus Rufungulo wakati akifanya maandalizi ya Kupanda Mlima Kilimanjaro ,shoto mwa Laswai ni Charity Githinji meneja masoko wa Kibo Palace.
Mfanyabiashara Vicent Laswai ambaye pia ni mkurugenzi wa Hotel za Kibo Palace akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufika kituo cha kwanza wakati wa kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia geti la Marangu,kituo cha Mandara akieleza matarajio yake mara baada ya kufika katika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: