Wednesday, March 11, 2015

DCB COMMERCIAL BANK WADHAMINI MASHINDANO YA TANZANIA BANKERS & PUBLIC FUNDS CUP‏‏‎

 Mkurugenzi Mtendaji  wa DCB  Commercial Bank Plc  Bw. Edmund Mkwawa akiongea na Waandishi wa Habari Makao makuu ya Benki ya  DCB
 
Benki ya DCB imethibitisha kushiriki katika Mashindano ya  Tanzania Bankers and Public Funds Cup 2015, hayo yalisemwa  na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bwana Edmund Mkwawa akiongea na waandishi wa Habari , alisema  Timu yao tayari imesha anza kufanya mazoezi ya kujiandaa na mashindano hayo tangu mwezi wa pili mwaka huu 2015 na kuwa timu ipo katika hari nzuri sana si kwa kushiriki tuu lakini pia kutoa upinzani mkubwa watakazokutana nazo na hata kunyakua kikombe.

 Pia Bwana. Mkwawa amesema kuwa DCB pamoja na kushiriki kwao lakini wameamua kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha kwa ufasaha zaidi na kuongeza kuwa lengo kubwa la DCB Commercial Bank kupitia udhamini na ushiriki wa mashindano hayo ni kupanua wigo mkubwa wa kimahusiano na kibiashara kwa ukaribu zaidi baina ya Benki,Mifuko ya kijamii na Jamii kwa ujumla. 

 Mwisho alitoa wito kwa wananchi mbalimbali kufika katika viwanja ambapo mashindano yatafanyika ili kujipatia Huduma Bora za Benki ya DCB na kujiunga na huduma mbalimbali zitolewazo na Benki hiyo katika Banda lao  maalum ambalo litakuwa katika viwanja hivyo.

Nae Mkurugenzi mtendaji wa My way Intertainment Bw. Paul Mganga alisema kuwa wanatarajia kuwa na mwitikio Mkubwa wa Taasisi za Kifedha na Mifuko ya Jamii katika Mashindano ya Tanzania Bankers Cup and Public Funds Cup 2015  kwa kujiunga na mashindano haya kama ilivyo DCB Benki ambao wameweza kuwa wa kwanza kuthibitisha wanashiriki mashindano hayo na Kudhamini pia na kuwashukuru kwa hilo.

Alihimiza kuwa Taasisi zengine za Kifedha na Mifuko ya Kijamii kuwa na mwitikio mkubwa wa mashindano hayo, kwani Michezo hujenga afya Bora na kukuza akili kama ilivyo kauli mbiu ya Mashindano haya"Tuungane katika Michezo, Michezo ni Afya , Michezo ni Ajira" Mwisho aliishukuru Benki ya DCB kuonesha mwamko mkubwa katika Swala la Michezo na kuomba Taasisi nyengine za Kifedha na Mifuko ya Jamii kuwa na mwamko huo.

Mashindano haya yanatarajiwa kuanza 28 Machi 2015 ambapo zaidi ya timu 18 kutoka taasisi za kifedha na Mifuko ya kijamii zitashiriki mashindano hayo kwa mfumo wa Ligi na mpaka sasa ni timu 11 ndizo zilizothibitisha kushiriki katika mashindano haya.
 Mkurugenzi Mtendaji wa My Way Entertainment Bw.  Paul Mganga akiongea na waandishi wa Habari Makao makuu ya DCB Commercial Bank.  
 Product Development and Marketing Manager wa DCB Commercial Bank Plc Bw. Boyd Mwaisame  akisisitiza  kuwa ndani ya viwanja vya michezo kutakuwa na Banda maalum la DCB Commercial Bank ambapo huduma mbalimbali za Benki hiyo zitatolewa eneo hilo.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya Tanzania Bankers and Pensions Funds Cup 2015 Bw. David Manoti alitoa wito kwa vyombo vya habari , wadau wa Michezo, na wananchi kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika mashindano haya. .
Mkutano na waandishi wa Habari  Makao Makuu ya Benki ya DCB ukiendele.

No comments: