Sunday, February 1, 2015

Mshindi wa milioni 100 za Jaymillions kukabidhiwa kitita cha fedha alizojishindia

Mshindi wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Uwezo Magedenge (22) akiwa nyumbani kwao kijiji cha Pamilini Kilolo Mkoa wa Iringa akiendelea na shughuri zake za nyumbani wakati alipotembelewa na maofisa wa Vodacom Tanzania kijijini hapo kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka jijini Dar es Salaam kwa makabidhiano rasmi ya kitita chake hivi karibuni.
Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (kulia) akimsikiliza kwa makini mshindi wa milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo Bi.Uwezo Magedenge (22) akimfafanulia jambo kuhusiana na ushindi wake,wakati alipomtembelea kijijini kwao Pamilini Kilolo mkoa wa Iringa kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka jijini Dar es Salaam, kwa makabidhiano rasmi ya kitita chake hivi karibuni.Wengine katika picha kushoto ni Mama yake mzazi Delfine Kisoma(64) na Baba yake Alatanga Magendenge (70).
Baba mzazi wa mshindi wa kwanza wa milioni 100 kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Alatanga Magendenge akimfafanulia jambo Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Matina Nkurlu(kulia) kuhusiana na ushindi wa mwanae Uwezo Magendenge(watatu toka kushoto)wakati alipomtembelea mshindi huyo nyumbani kwao kijiji cha Pamilini Kilolo Iringa kwa ajili ya kumchukua na kumpeleka Dar es Salaam kwa ajili ya kumkabidhi rasmi ya kitita chake hivi karibuni,kushoto ni mama mzazi wa mshindi Delfine Kisoma.
Mshindi wa Milioni 100/- kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Bi. Uwezo Magedenga (kushoto) akifurahia jambo na Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kulia)wakati alipofika kijijini kwao Pamilini Kilolo Iringa ili kujua mazingiara yake na kumpeleka jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kwa ajili ya kumkabidhi rasmi ya kitita chake hivi karibuni. Katikati ni Mkuu wa kampuni hiyo Kanda ya Kusini magharibi Amos Vuhahula.
Mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/-kuptia promoshe ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania, Uwezo Alatanga Magedenge (22) akifafanua jambo kuhusiana na ushindi wake wakati alipotembelewa na maofisa wa Vodacom Tanzania kijijini kwao Pamilini Kilolo Iringa.
Mshindi wa kwanza wa kitita cha shilingi milioni 100/-kupitia promosheni ya Jaymillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Uwezo Magedenga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wazazi wake,Alatanga Magedenga na Delfina Kisoma(kushoto) nje ya nyumba yao iliyopo katika kijiji cha Pamilini Kilolo mkoa wa Iringa .

Wazazi wa mshindi wa kwanza wa Sh Milioni 100 katika droo ya 14 ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom, Uwezo Magendenye (22) mkazi wa wilaya ya Kilolo wamesema kuwa wamefurahishwa na ushindi wa binti yao na watamshauri kuhakikisha anazitumia kuboresha maisha yao na kutimiza ndoto zake alizoshindwa kuzitimiza kutokana na  familia  aliyozaliwa kutokuwa na uwezo.

Baba mzazi wa  binti huyo, mzee Alatanga Madengenye (70),alionyesha furaha kubwa alipotembelewa na maafisa wa kampuni ya Vodacom  na kusema kuwa hatapenda kumuingilia kwenye matumizi ya pesa hizo japokuwa kama mzazi angependa kuona binti yake anatimiza na ndoto yake aliyoikosa kutoka na  hali ngumu ya maisha inayowakabili ambayo  ni kuhakikisha anapata  elimu bora.

“Binti yetu bado ni mdogo tuna imani kwa ushindi huu atarudi shule kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha”.Alisema Mzee Madengenye akiungwa mkono na mama yake mzazi Delfina Kisoma (64) alielezea furaha yake juu ya ushindi wa binti yake huyo akisema ni matarajio yao ushindi huo utasaidia kubadili maisha ya binti huyo na familia yao.

Akizungumza namna fedha hizo zitakavyobadili maisha yake, Uwezo Madengenye alisema kwa furaha na kujiamini alisema sasa ameamua kurudi shule kutafuta elimu  aliyoikosa kutokana  uwezo mdogo wa kifedha wa wazazi wake.“Ndoto yangu ya kurudia mitihani ya kidato cha nne iliyokufa miaka miwili iliyopita kutokana na uwezo mdogo wa familia sasa imefufuka. Nitarudi shule, nitasoma kwa bidii hadi nipate shahada ya chuo kikuu kama itawezekana,” alisema.

Alitaja matumizi mengine atakayofanya kuwa ni pamoja na kununua ardhi na kupanda miti, kukarabati nyumba ya wazazi wake na kusaidia ndugu zake ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za kimaisha ikiwemo kuanzisha biashara za aina mbalimbali ikiwemo  biashara ya  maduka ya M-Pesa na ikibidi kujenga nyumba yake ya kulala wageni .

Meneja Uhusiano wa Umma  wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alitembelea familia ya mshindi huyo akiongozana na Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi wa kampuni hiyo Amos Vuhahula  alisema binti huyo atakabidhiwa fedha zake jijini Dar es Salaam baada ya taratibu za makabidhiano kukamilika na aliwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hiyo kwa kuhakikisha wanatuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda.

Aliitaja njia nyingine ya kushinda kuwa ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo  mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-

Alisema tangu promosheni hiyo ianze mapema mwezi uliopitau tayari wateja 2  wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja  na  maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja, bado kuna mamilioni ya fedha yanawasubiri watanzania, wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha  kila siku wanaangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.

No comments: