Thursday, February 26, 2015

Balozi Seif Ali Iddi afanya ziara maalum ya kukagua shamba la Mkurunge,Bagamoyo

Meneja wa Shamba la Chuo cha Kilimo Kizimbani liliopo Makurunge Magamoyo Nd. Abdulrahman Mahmoud Hamid akimpatia maelezo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif wakati wa ziara yake ya kulikagua shamba la SMZ waliokabidhiwa chuo hicho.Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Ardhi Zanzib ar Mh.Abdulla Shaaban, Waziri wa Kilimo Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboyta na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nd. Ali Khalil Mirza.
Balozi Seif akitafakar na Mwanasheria wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa SMZ Bwana Saleh Said Mbarouk akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo kulia yake Nd. Hemed Mwanga mwenye miwani, Waziri wa Kilimo Bara Mh. Steven Wasira na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.
Baadhi ya sehemu ya shamba la Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Makurunge Bagamoyo ambalo limekabidhiwa Chuo cha Kilimo Kizimbani ili kuliendeleza.
Ujumbe wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar uliotembelea shamba la Mifugo la SMZ la Makurunge waliangalia fukwe ya Bagamoyo iliyomo pembezoni mwa shamba hilo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati na ujumbne wake wakifurahia fukwe safi iliyomo ndani ya shamba la Serikaliu ya Mapinduzi ya Zanzibar liliopo Makurunge. Kushoto ya Balozi Seif ni Meneja wa Shamba hilo Nd. Abdulrahman Hamid Mahmoud, wakati kulia ya Balozi Seif ni Katibvu Mkuu Wizara ya Kilimo na Mali Asili Zanzibar Nd. Afan Othman Maalim, Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, Waziri wa Kilimo Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwambioya na Naibu Waziri wa ARDHI Bara Mh. Angela Kairuki.
Naibu Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi Tanzania Bara Mh. Angela Kairuki akimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwamba Wizara hiyo itasimamia kukamilisha taratibu zote zitakazothibitisha uhalali wa umiliki wa SMZ katika shamba la mifugo la Makurunge Bagamoyo Mkoa wa Pwani. Kulia ya Naibu Waziri wa Ardhi Mh. Angela Kairuki ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo.  Picha na – OMPR – ZNZ.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba msimamo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Baraza lake la Mapinduzi wa kulitumia shamba lake la Kilimo liliopo Makurunge Bagamoyo Mkoa wa Pwani ni ule ule wa kuendeleza Mifugo na Kilimo.

Alisema uamuzi huo umezingatiwa kwa makusudi kuheshimu wazo la pamoja lililoibuliwa kati ya Rais wa Kwanza wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mwalimu Julius K. Nyerere na Rais wa Awamu ya Pili ya Zanzibar Mh. Aboud Jumbe Mwinyi la kuipatiwa Zanzibar eneo la Mifugo na Kilimo Tanzania Bara ili kuimarisha Sekta hizo.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati alipofanya ziara maalum ya kulikagua shamba la Mkurunge  akiambatana na Waziri wa Kilimo, Ushirika na Chula wa Bara  Mh. Steven Wasira, Naibu Waziri wa Ardhi Bara Mh. Angeja Kairuki, Waziri wa Ardhi Zanzibar Mh. Ramadhan Abdulla Shaaban, Waziri wa Kilimo Zanzibar Dr. Sira Ubwa Mwamboya, Makatibu Wakuu wa Wizara hizo pamoja na watendaji waandamizi wa Serikali zote mbili.

Alisema Shamba la Makurunge Bagamoyo lina Historia ndefu iliyoasisiwa na Marais waliopita ikilenga kuimarisha Muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar sambamba na kuipa nguvu Zanzibar kwa shughuli zake za kuongeza uzalishaji katika Sekta ya Mifugo.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Zanzibar imekuwa na eneo dogo la ardhi kwa kuendeleza sekta ya Kilimo na Mifugo huku idadi ya wakaazi wake ikiendelea kuongezeka kiwango ambacho kinastahiki kujengewa mindo mbinu ya maisha katika uzalishaji Kiuchumi.

Akitoa Taarifa ya Historia ya Shamba la Makurugne hapo Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo Mkuu wa Wilaya ya Magamoyo Nd.Majid Hemed Mwanga alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliomba eneo la ufugaji wanyama kwa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mapema mwaka 1977.

Nd. Mwanga alisema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Mali Asili ilitoa Barua rasmi Mwezi Febuari mwaka huo huo wa 1977 wa kuipatia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar eneo la Shamba hapo Makurunge Bagamoyo lenye ukubwa wa Hekta 28,099.

Alisema kazi hiyo ilikwenda sambamba na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwalipa fidia wananchi 64 waliokuwa na mali na vipando vyao kwenye eneo hilo ambapo watu 16 waliohusika na zoezi hilo walikataa kulipwa fidia hizo.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

No comments: