Sunday, January 4, 2015

DKT. MAGUFULI AWAPONGEZA CCM CHATO KWA USHINDI MKUBWA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA

Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwasalimia baadhi ya Wajumbe waa Chama cha Mapinduzi CCM waliofika katika hafla ya kupongezwa baada ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika hivi karibuni.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kulia akijadiliana jambo na Katibu wa CCM Wilaya ya Chato Hamis Mkaruka kuhusu mambo mbalimbali ya Chama.
Kijana wa kikundi cha Zeze kutoka Kata ya Kachwamba akitumbuiza kwenye mkutano huo wa kujipongeza kwa viongozi wa CCM Wilayani Chato.
Katibu wa CCM Wilaya ya Chato Hamis Mkaruka wakwanza kushoto akiwa na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Chato Rodrick Mpogolo wakipiga makofi wakati Kikundi cha Ngoma za Asili cha Zeze kutoka kata ya Kachwamba kikitumbuiza.
Wajumbe wa CCM Wilaya ya Chato wakijiandikisha katika mkutano huo wa kujipongeza mara baada ya Ushindi wa kishindo walioupata.
Wanachama wa CCM Chato wakicheza ngoma kusherekea ushindi huo.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akihutubia mamia wa wanachama wa CCM wilaya ya Chato waliojitokeza katika mkutano huo wa kupongezana.
Baadhi ya Wanachama wa CCM Chato wakiwa katika picha ya pamoja na Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mara baada ya Mkutano wao kumalizika.
Mbunge wa Chato ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akipakua wali kwa ajili ya wajumbe waliohudhuria mkutano huo wa kujipongeza kwa ushindi. Picha zote kwa Hisani ya Mwandishi Maalum-Chato.

No comments: