Wageni mbalimbali wakiingia na kutoka Katika Banda la Watanzania kujione bidhaa za Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Msanii wa kuchora Fred Halla akifanya sanaa yake ya Uchoraji katika Katika Banda la Watanzania.Fred ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Msanii wa Uchongaji Iddy Amana akiwahudumia wateja katika Banda la Watanzania. Iddy ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Mpishi wa Vyakula mbali mbali Haji Omar akiwahudumia wateja wake wanaopenda vyakula vya Kitanzania.Haji ni mmoja wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Baadhi ya Wateja wa Vyakula vya kitanzania wakila chakula chenye Asili ya Tanzania,Zanzibar (Urojo) katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman.
Mkuu wa Msafara wa Watanzania Wanaoshiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa,Ubunifu na Utamaduni yanayoendelea Mascut-Oman Bi Khadija Bhatashy akiulizia bei ya bidhaa katika Banda la Iran. Iran ni moja ya nchi washiriki wa Maonesho hayo. Picha na Faki Mjaka-Mascut Oman.
Na Faki Mjaka-Mascut Oman
Kukosekana kwa Semina ya pamoja na uelewa mdogo wa lugha ya Kiarabu ni miongoni mwa Changamoto zinazowakabili Wajasiriamali wa Kitanzania wanaoshiriki Maonesho ya Kimataifa ya Sanaa na Utamaduni nchini Omani.
Hayo yameelezwa na Watanzania wanaoshiriki Maonesho hayo yanayoendelea kwa muda wa mwezi mmoja na kushirikisha Mataifa mbalimbali.
Mmoja ya Wajasiriamali hao Kulthum Mohamed amesema uelewa mdogo wa lugha ya Kiarabu ni changamoto kwake inayomkabili katika kutoa ufafanuzi wa baadhi ya Bidhaa alizokuwa nazo.
Mjasiri Amali huyo wa Viungo (spices) amedai kuwa licha ya baadhi ya Waarabu kujua Lugha ya Kiswahili amebaini hawapendi kuzungumza jambo ambalo linawapa shida.
“Licha ya hawa WaomanI kukijua Kiswahili lakini wengi wao wanavyofika hapa wanajifanya hawakijui jambo ambalo linatukwaza kidogo katika kutoa ufafanuzi wa Bidhaa zetu kwa Lugha ya Kiarabu” Alisema Kulthum.
Aidha K amebaini kuwa hakukuwa na Semina ya Pamoja ya Washiriki kujua mambo mbalimbali na Vipaumbele vya Waarabu jambo ambalo lingeweza kuwajengea uelewa mpana wa Waoman nakujua Bidhaa muhimu zaidi za kuja nazo katika Maonesho hayo.
Kwa upande wake Mkuu wa Msafara huo wa Watazania katika Maonesho hayo ya Utamaduni na Sanaa Bi Khadija Battashy amesema kuna baadhi ya Bidhaa ambazo haziendani sana na Utamaduni wa Omani kama vile nguo za kike zenye Mikono Mifupi.
“Kwa mfano utakuta baadhi ya Nguo tulizokuja za kike nyingi zao zimetengenezwa zikiwa na Mikono mifupi tena zimepasuliwa sasa kwa Utamaduni wao hawa hawazipendelei sana,nadhani tungetengeneza za Mikono mifupi Wangezipenda zaidi” Alisema Bi Khadija Battashy.
Hata hivyo anaamini Tanzania itafanya vyema katika Monesho hayo na hata kuibuka Mshindi wa mwanzo ikiwa kutatokea kutangazwa mshindi.
Kwa upande wake Mjasiriamali wa Bidhaa za Nguo Bi Anna Matinde amesema ana matumaini makubwa kuwa Bidhaa za Tanzania zitapata Wateja kutoka na ubora wake.
“Mi naamini Bidhaa zetu ni bora na zitapata Wateja maana hata hiyo Mishahara ya Waarabu bado tunaamini ikitoka watazidi kununua bidhaa zetu” Aliongeza Bi Anna.
Kwa Upande wao Wageni wanaolitembelea Banda la Tanzania wamelisifia kutokana na kuwa na bidhaa bora na za upekee zikiwemo za Viungo kama vile Karafuu na Mavazi ya Kimasai.
Maonesho hayo ya Muda wamwezi mmoja ya Sanaa, Ubunifu na Utamaduni yanayofanyika katika Jimbo la Al-Amerat mjini Mascut, huanza kila ifikapo saa 10 jioni na kufungwa saa nne usiku kwa Majira ya Oman ambapo Nchi mbalimbali Washiriki huonesha Bidhaa zilizotengenezwa kwa Mikono zinazowakilisha Utamaduni wao na Watu hununua Bidhaa hizo.
No comments:
Post a Comment