Tuesday, October 21, 2014

TANZANIA KUANIKIZA MAFANIKIO YA Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) KWA MATAIFA manane

DSC_0012
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na washiriki wa mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.(Picha zote na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi wetu
MATAIFA manane  yaliyopo katika nchi zinazoendelea zitaanikizwa mafanikio ya Tanzania katika utekelezaji wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) inayosimamiwa na  Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF).
Pamoja na upelekaji wa maarifa yaliyopatikana nchini Tanzania katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mradi huo ambao ulianza mwaka 2012 na kumalizikia 2015, Watanzania ndio watakaotumika kupeleka maarifa mapya.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa ushauri wa ufundi wa UNCDF, Peter Malika wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha ya siku tatu inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau mbalimbali wanaohusika na programu hiyo.
Wadau hao ni waandaaji wa miradi, watoa fedha na wasimamizi wanaofanya maamuzi.
Alisema baada ya mafanikio ya mradi huo, UNCDF imemua Tanzania kuwa makao makuu ya LFI na kwamba watanzania baada ya kuonesha uwezo wa dhana za LFI, mafanikio hayo katika mataifa mengine.
Mataifa yaliyoelezwa kupelekewa utaalamu wa watanzania kuanzia awamu ya pili inayotarajiwa kuanza mwakani hadi mwaka 2017 ni Uganda, Benin, Senegal na Bangladesh.
DSC_0081
Majadiliano ya nchi nyingine tatu bado yanaendelea na zitapatikana baada ya serikali hizo kukubali kuwepo kwa mradi huo, alisema Malika.
Alisisitiza kwamba program ya LFI inatekelezwa kwa kushirikiana na serikali na hapa Tanzania inafanyika kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI).
Katika utekelezaji wa program hiyo LFI imesaidia miradi kadhaa yenye kipaumbele inayogusa miundombinu ya nishati, kilimo na mawasiliano.
Kwa mujibu wa Malika kuna miradi 25 yenye maslahi kwa umma ambayo imewezeshwa kutekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.
Akifafanua zaidi alisema miradi hiyo 25 ya miundombinu iliyoanzishwa na wawekezaji wa umma na binafsi iko katika hatua mbalimbali za uendelezaji.
Aidha alisema miradi hiyo imetawanyika katika sekta mbalimbali zikiwemo za usindikaji bidhaa za kilimo, nishati, miundo mbinu ya utoaji huduma za jamii, mawasiliano na uzalishaji viwandani katika mikoa 10 kote nchini.
DSC_0125
Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner akitoa mada yenye kuainisha zana za ubunifu zikiwemo masuluhisho wakati wa uhaba wa fedha, mkakati ya kukabili athari, mtiririko wa uandaaji mikataba na masharti na kanuni za msingi zinazoweza kujitokeza katika kila mkataba kwenye warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandazi wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
Hadi kufikia Septemba mwaka huu miradi mitano iliyopiga hatua kubwa zaidi ilitarajiwa kufikia kikomo cha bajeti yake katika miezi sita hadi tisa ijayo ambapo dola milioni 26 za mtaji wa ndani katika muundo wa mkopo na misaada ipatayo dola milioni 3 ilihamasishwa.
Msaada wa LFI kwa miradi iko katika muundo wa utaalamu wa kiufundi, kutoa amana, misaada ya kifedha na aina nyingine ya mikopo ambayo inahitajika sana kwa miradi midogo na ya kati ya miundombinu ili ivutie uwekezaji.
LFI imeundwa kuhamasisha ukuaji endelevu, jumuishi na wenye usawa kwa kufungua fursa za uwekezaji ili kuleta mabadiliko chanya na kusaidia miradi kupata fedha kupitia sekta binafsi na hasa masoko ya mitaji.
UNCDF yenye jukumu la pekee kuhusiana na fedha katika mfumo wa Umoja wa Mataifa, shirika hili limelenga kutoa msaada wa mtaji wa kuwekeza na wa kiufundi katika seklta ya umma na binafsi.
Aidha imepewa uwezo wa kutoa fedha za uwekezaji katika muundo wa misaada, mikopo na uwezeshaji wa ukopaji na utaalamu wa kiufundi katika kuandaa taarifa ya mradi kuhusu uendelevu na kujenga uwezo wa kuondoa hatari ya kuporomoka.
DSC_0095
Kazi ya UNCDF ni kuhakikisha pia watu katika mikoa na maeneo yote wananufaika na ukuaji wa uchumi kwa kushughulikia changamoto zao hasa maeneo ya pembezoni mwa mji na  vijiji.
Na katika hilo Malika alisema lengo kuu ni kuhakikisha kwamba miundombinu hasa ya maeneo ya vijijini ambayo haiwezi kupata kirahisi ridhaa ya taasisi za kifedha au utekelezaji wa serikali kuu inawezeshwa kwa kuitafutia andiko madhubiti na kuelekeza namna ya kupata fedha za utekelezaji.
“Kwa maneno mengine, miradi ile ambayo pengine isingekopesheka athari zake zinapunguzwa na kuingizwa katika hatua ya kuwa tayari kupokea uwekezaji ambapo inaadaliwa ili ipate mtaji wa kibiashara” alisema Malika.
DSC_0210
Mkurugenzi wa Nelwa's Gelato wauzaji wa watengenezaji wa Ice Cream, Bi. Mercy Kitomari akiuliza swali muwasilishaji mada Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner wakati wa warsha hiyo.
Matokeo ya jumla ya LFI, kwa mujibu wa Malika ni kuongezeka kwa ufanisi wa rasilimali fedha kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya hapa nchini kupitia uhamasishaji kwanza kabisa wa mtaji binafsi kutoka nchini na masoko ya mitaji ili kuwezesha na kuhamasisha maendeleo ya mahalia yaliyo jumuishi na endelevu.
Akizungumzia warsha hiyo ya siku tatu ambayo imeanza leo, Malika alisema kwamba zaidi ya watu 120 watashiriki wakiwamo waandaaji miradi na taasisi za kifedha.
Mafunzo ya leo ambayo yalihusu waandaaji miradi waliwezeshwa na mtaalamu nishati mbadala Michael Feldner ambaye pia ni mshauri wa masuala ya kifedha wa UNCDF.
Mtoa mada huyo aliainisha zana za ubunifu zikiwemo masuluhisho wakati wa uhaba wa fedha , mkakati ya kukabili athari, mtiririko wa uandaaji mikataba na masharti na kanuni za msingi zinazoweza kujitokeza katika kila mkataba.
Mafunzo mengine yatagusa watu wa fedha wanaopokea maandiko na kuyafanyia tathmini, ambayo yatafanyika kesho na kuishia na watoa maamuzi katika taasisi hizo kuhusu mikopo iliyoombwa.
DSC_0228
Mtaalamu wa masuala ya fedha wa programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) Abraham Byamungu akitoa ufafanuzi kwa washiriki wa warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
DSC_0117
Kutoka kushoto ni Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Bw.  Peter Malika, Bw. Imanuel Muro wa UNCDF pamoja na  Ofisa Msaidizi anayeshughulikia masuala ya fedha Program ya LFI kutoka UNCDF, Bw. Oscar Kanyenye wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa na Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner (hayupo pichani).
DSC_0083
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na mfuko huo katika hoteli ya Serena mjini Dar es salaam leo.
DSC_0138
DSC_0120
DSC_0122
Washiriki wa warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) wakisikiliza mada katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
DSC_0209
Mshiriki kutoka Ileje Mbeya, Bw. Joseph Mchome akitoa maoni yake kwenye warsha ya siku 3 ya mafunzo ya uandaaji wa miradi chini ya programu ya Jitihada za Mahalia za Utafutaji Fedha (LFI) unaosimamiwa na Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF) katika hoteli ya Serena mjini Dar es Salaam leo.
DSC_0187
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akizungumza na waandishi wa habari kuhusu warsha ya siku tatu inayofanywa na UNCDF iliyolenga kuwaelimisha wadau mbalimbali wanaohusika na programu hiyo.
DSC_0168
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akibadilishana mawazo na Mtaalamu wa nishati mbadala na mshauri wa masuala ya kifedha wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Michael Feldner kwenye warsha hiyo.

No comments: