Monday, October 20, 2014

AFRIKA KUSINI WATWAA UBINGWA WA SAFARI POOL AFRIKA 2014

TIMU ya Taifa ya mchezo wa Pool ya Afrika Kusini Wanaume imeibuka na ubingwa wa Afrika katika mashindano ya Pool yaliyojulikana kwa “Safari Lager All Africa Pool Championship 2014” yaliyofanyika katika Ukumbi wa Budget jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na hivyo kujinyakulia zawadi ya Dolla 5,0000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 8,500,000/= pamoja na medali za dhahabu.

Mashindano ya mwaka huu yaliendeshwa  kwa mfumo wa Ligi ambapo afrika Kusini walipata ubingwa kwa kuongozwa kwa Pointi 12,wakatiti waandaaaji wa mashindano kwa mwaka 2014, Tanzania walipata pointi 10 na hivyom kuzawadiwa dolla za kimarejkani 2,000$ pamoja na medali za silva wakifuatiwa na Zambia mabingwa watetezi pointi 9 ambao walikamata nafasi ya tatu na kuzawadiwa medali za shaba, ambapo Uganda nafasi ya nne walipata pointi 7 na  Kenya walipata nafasi ya tano kwa pointi 2.

Upande wa Wanawake pia timu ya Afrika kusini ilitwaa ubingwa kwa pointi 11 na kuzawadiwa medali za dhahabu, nafasi ya pili ilichukuliwa na Uganda kwa pointi  8 na kuzawadiwa medali  za silva, nafasi ya tatu ilikwenda kwa Tanzania ambao walipata pointi 5 na Kenya ilikamata nafasi ya nne kwa pointi 0.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume, IshmaelMthethwa kutoka Afrika Kusini alitwaa ubingwa huo na hivyo kuzawadiwa dolla 2,000$ pamoja na Medali ya dhahabu wakati mshindi wa pili ni Aden Joseph kutoka Afrika Kusini pia ambaye alizawadiwa dolla 1,000$ pamoja na medali ya silva.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Nkosi Sikelel’l kutoka Afrika  Kusini alifanikiwa kutwaa  ubingwa  na hivyo kuzawadiwa dollah 1,000$ pamoja na medali ya dhahabu wakati mshindi wa pili ni Rose Deus kutoka Tanzania ambaye alizawadiwa dolla 5,00$ pamoja na medali ya silva.

Akizungumza na wanamchezo pamoja na wadau wa pool  Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alishukuru kwa mashndano kwanza kufanyika Tanzania kwa mara ya kwanza na pia alishukuru kwa mashindano kuisha salama bila matatizo yeyote.

Shelukindo aliipongeza timu ya Taifa ya Afrika Kusini kwa kutwaa ubingwa wa Afrika kwa mwaka 2014 lakini pia aliipongeza timu ya Tanzania kwa kupiga hatua mpaka nafasi ya pili upande wa timu na nafasi ya pili kwa kina dada singles.

Meneja Oscar aliwaomba  zwachezaji kuongeza  juhudi katika mazoezi na ikiwezekana mwaka ujao wa 2015 tuwe mabingwa wa Afrika kama ilivyo bia ya Safari Lager bia bora Afrika.

Nae Rais wa Chama cha Pool Afrika(AAPA), Saths Reddy aliipongeza Tanzania kwa makaribisho mazuri na maandalizi mazuri na kukiri kwa mara zya kwanza mashindano ya Afrika ya Mwaka huu 2014 yaliyoandaliwa na Tanzania yamekuwa na hamasa na ushindani wa hali ya juu na hiyo inaonyesha kuwa mchezo wa Pool sasa umekuwa.

Mwisho Rais aliwatakiwa kila nchi kurudi nyumbali salama na mashindano ya mwaka 2015 yatakuwa Lethoto hivyo aliwaomba Tanzania kupitia mzamini Safari Lager wasikose kushiriki.
Mabingwa wa Safari Pool Afrika 2014 kutoka Afrika Kusini, timu ya Taifa ya Pool ya Nchi hiyo wakishangilia na kitita cha Dolla 5000$ sawa na pesa taslimu za Kitanzania Shilingi 8,500,000/= pamoja na medali za dhahabu baada ya kutwaa ubingwa huo uliojulikana kwa “Safari All Africa Pool Championship 2014” uliomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaaam.
Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Meneja wa timu ya Taifa ya Afrika Kusini ya mchezo wa Pool, kitita cha Dolla 5000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 8,500,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Rais wa Chama cha Pool Africa(AAPA), Saths Reddy(kulia) akimkabidhi Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania ya mchezo wa Pool kitita cha Dolla 2000 sawa na pesa taslimu za kitanzania 3,400,000/= mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Wachezaji wa Taifa wa mchezo wa Safari Pool Tanzania, wakishangila wakiwa na kitita cha Dolla 2000$ sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali za Silva mara baada ya kuibuka washindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles), Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles), Ishmael Mthethwa kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 2,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 3,400,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Suzette Booyens(kulia) kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 1,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 1,700,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Suzette Booyens(kulia) kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 1,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 1,700,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.
Bingwa wa Afrika wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Suzette Booyens(kulia) kutoka Afrika Kusini akionyesha kitita cha Dolla 1,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 1,700,000/= pamoja na medali ya Dhahabu mara baada ya kuibuka bingwa katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam.
Msindi wa Pili wa Tanzania wa mchezo wa Pool upande wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Wanawake, Rose Deus(kulia) akionyesha kitita cha Dolla 5,000 sawa na pesa taslimu za kitanzani Shilingi 850,000/= pamoja na medali ya Silva mara baada ya kuibuka msindi wa pili katika mashindano ya mchezo huo yaliojulikana kama “Safari All Africa Pool Championship 2014” yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa Budget Kunduchi Beach jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo.

No comments: