Tuesday, September 23, 2014

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA MKUTANO WA ELIMU: KUWAWEZESHA VIJANA KUFANYA MAAMUZI SAHIHI YA KIAFYA BARANI AFRIKA

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya kiafya.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller wakati wa mkutano wa kuzungumzia masuala ya elimu kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi ya kiafya barani Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (wa pili kulia) na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika (wa pili kushoto). Aliyesimama wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi na wa kwanza kushoto ni Msaidizi wa Mke wa Rais wa Malawi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya masuala ya elimu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo ni sehemu ya Maandalizi ya Mkutano wa Mwaka wa Marais na Wakuu wa Nchi za Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya washiriki kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika ili wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama Salma Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa na wageni wengine mashuhuri wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani. Aliyekaa wa kwanza kushoto ni Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller akifuatiwa na Mama Getrude Mutharika na wa kwanza kulia ni Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Vijana Bwana Ahmed Alhendawi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Rais Malawi Mama Getrude Mutharika mwishoni mwa mkutano wa kujadili masuala ya elimu kwa vijana barani Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Aliyesimama katikati ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dkt. Sheila Tlou, Mkurugenzi wa UNAIDS – Regional Support Team for Eastern and Southern Africa na Waziri Mstaafu wa Afya wa Botswana na kushoto ni Mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika mara baada ya kumalizika mkutano wa siku moja uliofanyika huko New York tarehe 22.9.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI.

No comments: