Saturday, August 23, 2014

Matukio mbalimbali mjini moshi leo

Askari wa Kikosi cha usalama barabarani aliyefahamika kwa jina la Anna Sawani akichukua maelezo toka kwa dereva wa gari la shirika la Umeme (TANESCO) baada ya kumgonga dereva wa boda boda.
Pikipiki ya dereva wa boda boda baada ya kugongwa wakati akijaribu kukata kona katika maungio ya barabaraba mbili maarufu kama Double road ,
Baadhi ya wananchi wakitizama majeruhi wa ajali hiyo.
Wasamaria wema wakijaribu kumbeba dereva wa boda boda kwa ajili ya kumkimbiza hosptali baada ya kuogongwa.
Abiria aliyekuwa katika pikipiki hiyo akipatiwa huduma ya kwanza.
Wakati wengine wakijaribu kuokoa majeruhi katika ajali hiyo ,vibaka wakatumia fursa hiyo kuwaibia wananchi waliokuwa katika eneo hilo kama anavyoonekana kijana huyu akipokea kichapo baada ya kukamatwa akiiba radio.
Baadaye wananchi wakataka kumpiga kiberiti kijana huyo baada ya kuanza kumuwekea majani na maboksi.
Kijana huyo akatoa utetezi wake kadri alivyoweza ya kuwa hakuiba radio,huku akiomba msamaha na kuahidi kuonesha nani aliyeiba.
Hatimaye akasamehewa na kuepuka kiberiti.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

No comments: