Tuesday, July 22, 2014

PROF. MARK MWANDYOSA AFANYA ZIARA YA KIKAZI MAKAO MAKUU YA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA (TCAA) JIJIJI DAR

Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) Dk. james Diu( Kulia ) akifafanua jambo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya wakati alipotembelea makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli zinazofanywa na TCAA.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya akikabidhiwa Nyaraka ya Sheria ya Mamlaka ya Usafiri wa Anga TCAA na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Dk. James Diu , wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya ofisi hiyo jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa hapo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum , Prof Mark Mwandosya, akisisitiza jambo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wakati alipokutana na Uongozi wa Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) Dk. james Diu.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kiusalama wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), akifafanua wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya Makao Makuu ya TCAA jijijni Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya akimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Rubeni Ruhongore wakati alipokuwa akimuelezea shughuli zinazofanywa na TCAA wakati Waziri huyo alitembelea Makao Mkuu ya Mamlaka hiyo kwa ajili ya ziara ya kujionea shughuli zinazofanywa na Mamlaka hiyo.
Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini –(SUMATRA) David Mziray akifafanua jambo wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya TCAA makao makuu.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu , Mamlaka ya Usafiri wa Anga(TCAA) Dk. james Diu( Kushoto)akiagana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Prof. Mark Mwandosya mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi makao makuu ya Mamlaka hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya kujionea shughuli mbambali zinazofanywa na TCAA. Kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA, Rubeni Ruhongore.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Kazi Maalum, Prof. Mark Mwandosya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) na Mamlaka zingine za Udhibiti Nchini wakati alipotembelea Makao Makuu ya TCAA, Dar es Salaam.

No comments: