Thursday, June 26, 2014

HALMASHAURI ZATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO MIRADI YA MAENDELEO

IMG-20140625-WA0044
Mkurugenzi  Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42)  unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB)uliyofanyika  jijini Arusha
IMG-20140625-WA0045-1
Mkuu wa Mkoa Arusha Magessa Mulongo akiongea katika uzinduzi huo
IMG-20140625-WA0040Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa
20140624_214539Kulia Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema katikati Mkuu wa Wilaya ya Arusha John Mongela na mkurugenzi wa jiji  la Arusha
20140624_222604Washiriki katika uzinduzi huo
20140624_222551
IMG-20140625-WA0042
IMG-20140625-WA0039Meja Stepher Mtaheba wa kikosi cha jeshi  akijitambulisha katika uzinduzi huo
IMG-20140625-WA0038IMG-20140625-WA0043
HALMASHAURI mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wananchi wametakiwa kutoa ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.
 
Aidha kumekuwepo na changamoto mbalimbali ambazo zimekuwa zikikwamisha miradi hiyo ikiwemo ya wananchi kukataa kulipwa fidia kwa taratibu za sheria za nchi ili kutoa maeneo ya kuchimbwa changarawe, kokoto na kuchota maji.
 
Hayo yalisemwa juzi na Mkurugenzi  Mkuu wa wakala wa barabara (TANROADS) ,Injinia Patrick Mfugale wakati akizungumza katika uzinduzi wa mradi wa Arusha-Holili /TAVETA –VOI kilometa 122 pamoja na Arusha –bypass (km 42)  unaofadhiliwa na benki ya maendeleo ya Afrika (ADB) uliofanyika katika ukumbi wa naura springs mjini hapa.
 
Alisema kuwa,kumekuwepo na changamoto kubwa sana zinazosababishwa na wananchi na baadhi za halmashauri katika utekelezaji wa miradi hiyo hali ambayo imekuwa ni kikwazo kikubwa katika kufikia malengo yaliyowekwa.
 
Alifafanua  kuwa, halmashauri za wilaya pamoja na serikali za vijiji wamekuwa wakitoza kodi mbalimbali kwa vifaa vya ujenzi kama kifusi, mchanga,kokoto,na maji.
 
Mfugale alisema kuwa,mradi wa ujenzi wa barabara ya Arusha-holili ni sehemu ya mradi wa kimataifa unaojulikana kwa jina la Holili/Taveta –Voi unaounganisha nchi yetu na nchi jirani ya Kenya utagharimu kiasi cha dola za kimarekani milioni 223.
 
Alisema kuwa, awamu ya kwanza ni kuijenga kwa njia nne sehemu ya barabara kutoka Sakina –Tengeru (km 14.1) na Arusha bypass (km 42) kwa fedha za mkopo kutoka ADB .
 
Aliongeza kuwa, sehemu ya pili ni kuendeleza ujenzi wa njia nne kutoka Tengeru hadi Usa river (km 8.2) na ukarabati wa sehemu ya barabara iliyobaki hadi Holili baada ya kupata fedha.
 
Naye Mwakilishi wa benki ya maendeleo ya Afrika (ADB), Injinia Patrick Musa  alisema kuwa kumekuwepo na changamoto kubwa ya hali ya hewa ambayo imekuwa ikichangia mradi kukamilika kwa wakati na ucheleweshaji wa ulipwaji wa fedha za wakandarasi .
 
Alisema kuwa, wao kama benki ya maendeleo ya Afrika wataendelea kutafuta hela kwa ajili ya maendeleo kwani ni fursa nzuri wao kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuleta maendeleo.(jamiiblog Pamela  Mollel)

No comments: