Saturday, May 24, 2014

Dkt.John Magufuli aongoza zoezi la Kuapishwa kwa Wahandisi

Waziri wa Ujenzi Mhe.Dkt.John Magufuli Leo ameongoza zoezi la Kuapishwa kwa Wahandisi zaidi ya 100 (Kiapo cha uaminifu katika kazi yao)katika hoteli ya African Dream Mjini Dodoma.
Zoezi la kuwaapisha Wahandisi hao limefanywa na Hakimu Mkazi Mhe.Verynice Kawishe na Kusimamiwa na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA) Mhe.Donald L.Chidowu.
Walio walioapishwa ni Wahandisi Viongozi kumi, walioapishwa mmoja mmoja. Kundi hili likijumuisha Makatibu wakuu Manaibu na Wabunge. Kundi la pili ni Wahandisi mia moja ishirini ambao walikula kiapo cha Pamoja.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhe. Eng. Gerson Lwege akiapishwa. Pichani kutoka. kushoto, Msajili wa Bodi ya Makandarasi Eng.Steven D.M.Mlote,Mwenyekiti wa Makandarasi,Eng.Pfrof.Ninatubu Lema,Waziri wa Ujenzi Mhe.John Magufuli ,Hakimu Mkazi Mhe.Verynice Kawishe na Wakili Mkuu wa Serikali (PSA) Mhe.Donald L.Chidowu.
 Naibu Waziri wa  Uchukuzi,Mhe. Eng.Dkt.Charles Tizeba akipongezwa na Mhe. Dkt John Magufuli mara baada ya kuapishwa.
 Wahandisi viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na Hakimu Mkazi   Mhe.Verynice Kawishe wakati akiapisha Wahandisi 120 kwa pamoja.
 Wahandisi wakiwa wanaapa kwa pamoja.
 Wahandisi wakiwa wanaapa kwa pamoja.
 Wahandisi wakiwa katika picha ya Pamoja kwa makundi manne tofauti mara baada ya kula  kiapo cha uaminifu katika kazi yao ya Uhandisi.


No comments: