Thursday, October 31, 2013

BAADHI YA WAANDISHI WA HABARI KUTOKA TANZANIA NA KENYA WAFANYA ZIARA KWENYE WONDER CAVES,NCHINI AFRIKA KUSINI

 Muongozaji wa Wataalii,Marinus Hurter akitoa maelezo kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi za Tanzania na Kenya waliofanya ziara kwenye mapango ya Cradle of Humankind and Wonder,yaliopo katika mji wa Gauteng nje kidogo ya Jiji la Johannesburg Afrika Kusini.Waandishi hao wapo nchini Afrika kusini kwa ziara ya wiki moja kwa hisani ya Bodi ya Utalii ya Afrika Kusini.
Maelezo kuhusiana na historia ya Mapango hayo.
 Baadhi ya waandishi wa habari kutoka nchi za Tanzania na Kenya wakifanya ziara kwenye mapango ya Cradle of Humankind and Wonder,yaliopo jijini Johannesburg,Afrika Kusini mapema leo asubuhi.
 Sehemu ya Mabaki ya Reli yaliopo ndani Mapango hayo,yakikadiriwa kuwepo kwa zaidi ya miaka 100. 

Moja ya nondo iliyokuwa ikitumiwa na watu wa zamani ndani ya Mapango hayo,ikiwa ni sehemu ya kutimba Mawe ya Chokaa.Waandishi hao wapo nchini Afrika kusini kwa ziara ya wiki moja kwa hisani ya Bodi ya Utalii ya Afrika Kusini.
 Muonekano wa vivutio mbali mbali ndani ya Mapango hayo. 
 Waandishi wa Habari waliopo kwenye ziara hiyo wakiendelea kupatiwa Maelezo.
 Baada ya ziara ndefu ndani ya Mapango ya Cradle of Humankind and Wonder.
Mie pia nipo kwenye ziara hiyo na hapa tukiwa na Muongoza Watalii,Marinus Hurter (kati) na kulia ni Mdau Anganile.
 Hii ni sehemu ya njia ya kuingia ndani ya Mapango hayo.
ngazi.

YALE YALEEEE........

 Mmoja wa wakazi wa mtaa huu aliye amua kujitoa na kushika kinyesi ili apate kuzibua chemba ambayo ilikuwa inamwaga maji bila kusimama kwa siku Sita katika mtaa wa Mwenge jijini Dar es salaam.
 Hali hii ilikuwa mbaya jambo ambalo wananchi waliamua kujitolea na kufanya wawezalo ili kuzibua 
 Hali ni Tete eneo Hili ambapo sasa moja ya Chemba inazidi mwaga maji.. hapa kila mtu anatoa wazo lake nini kifanyike ili kuweza kuzibua eneo hilo ambalo maji yake yalikuwa hayapungui kumwagika bali kuongezeka..na mwisho wote waliona bora washike kinyesi kuliko kuendelea kuteseka. 
 Ilikuwa ni Baada ya Kuhangaika sana wakazi wa eneo hili kwa kutumia nyenzo yao Duni ya nondo maalumu ya kuzibulia chemba waliyo jinunulia wenyewe  , hatimaye walifanikiwa kuzibua chemba moja na kuhamia chemba ya pili .
 Baada ya Chemba ya Juu kuzibuka , kasheshe ikahamia katika chemba ya pili ambapo sasa maji yote yalihamia hapo.
 Masikini mtazame Mama huyu alivyo Ruka juu na mtoto akiwa amemshika kihatari namna hii... hii ni adha ya haya maji taka.
 Wakazi wa eneo hili wakiwa wanakomaa kwa nguvu zote kuanza kuzibua chemba ya pili.
 Zoezi sasa linaendelea na hapa walikuwa wanaendelea kuzibua chemba ya 3 ambapo sasa  walifika kikomo baada ya kuonekana chemba hiyo ilikuwa imejaa matakataka ya kutosha pamoja na Mchanga . Na ndipo walipo pata taarifa kuwa DAWASCO wanakuja.
Wakiwa wamefika  kabisa na kujionea Adha ya kukanyaga maji Taka ...... huo nyuma ni mtambo maalum wa kuzibua Chemba 
 Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wamefika katika eneo la tatizo na kuanza kuzibua chemba za maji taka ili kuwasaidia wakazi hao wasipatwe  na magonjwa , Kero ya maji mtaani na Harufu mbaya
 Wakiwa wanahakikisha kabisa kwamba tatizo limekwisha eneo hilo...
 Moja ya Chemba ambayo wakazi wa Mwenge walikuwa wamehangaika nayo sana mpaka kufanikiwa  kutoa maji taka hayo  yaende ikiwa inaangaliwa na wafanyakazi wa DAWASCO
 Wafanyakazi wa DAWASCO wakiwa wanaendelea kutoa takataka katika chemba sugu ili kuruhusu maji yapite 
 Hii ni Baada ya Chemba Kuzibuliwa na wananchi wakishirikiana na DAWASCO Ambao walichelewa kufika eneo la tukio
 Maji yakionekana yanaendelea kukauka baada ya Chemba hizo kuzibuliwa 
Hizi ni Takataka zilizo bakia baada ya kuzibua Chemba hizo ... 
Wananchi mtaa wa mwenge  waandamana na kufanya usafi kufuatiwa na kero kubwa iliyokuwa sugu na hatari katika afya zao, kero hiyo ikiwa ni kuziba na kufumuka  kwa chemba zinazo pitisha maji machafu maarufu kama  (majitaka )
Ikiwa nizaidi ya wiki mbili wakazi na watumiaji wa njia ya mwenge katika mtaa huo uliogeuzwa jina na kupewa jina mahususi na mazingira ya mtaa ambalo ni mtaa wa( kinyesi street) wamekumbwa na kero ya kufumuka kwa chemba za  maji taka na kuwa na harufu mbaya  hivyo wananchi wamehofia afya zao nakuanza kuzibua Chemba za maji hayo huku kila baada ya mwezi huletewa  Bili na kuweza kuzilipia bila ya wasiwasi .Lakini kibao kimegeuziwa kwa wananchi kuwa ndio wamiliki wa shirika la maji safi na taka (DAWASCO) leo hii waamua kuondoa adha hiyo iliyo dumu kwa muda mrefu bila ya ufumbuzi kwa kushika Kinyesi na maji machafu kutoka sehemu mbalimbali.
Hata hivyo wakazi walilalamika kuhusu  utendaji kazi wa dawasco kuwa ni mbovu kwa kuwa wame watafuta zaidi ya mara kadhaa  bila mafanikio
Aidha wananchi walionekana kuwa na moyo mmoja wa ushirikiano kufuatia harufu mbaya iliyokuwa ikitoka katika chemba hizo nakufanikisha kuzibua chemba zote katika mazingira magumu yanayo weza kusababisha maradhi mbalimbali kwa jamii husika wameongeza kuwa wana iomba mamlaka ya maji (DAWASCO) hususani kitengo cha majitaka kuweza kupita kila baada ya wiki moja ili kuweka mazingira mazuri/safi. PICHA NA DAR ES SALAAM YETU

tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week lafana sana mjini Pretoria, Afrika Kusini

Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa wa nchini Afrika ya Kusini, David Tlale akiwa na Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania,Millen Magesa wakipita stejini mara baada ya kuonyesha mavazi yake katika tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week lililofanyika kwenye Stesheni ya Treni ya Rovos, Mjini Tshwane,Pretoria nchini Afrika Kusini
Mwanamitindo wa Kimataifa kutoka nchini Tanzania,Millen Magesa akipita Stejini kuonyesha mavazi yaliyobuniwa na Mbunifu wa mavazi wa Kimataifa wa nchini Afrika ya Kusini, David Tlale wakati wa onyesho lililofanyika usiku wa kumamkia leo kwenye Stesheni ya Treni ya Rovos,Mjini Tshwane, Pretoria nchini Afrika Kusini.
 Wanamitindo mbali mbali wa nchini Afrika Kusini wakipita na mavazi ya aina mbali mbali stejini wakati wa tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week.
 Wadau kutoka sehemu mbali mbali wakihudhulia tamasha la Mercedez Benz African Fashion Week. 
Chief Photographer wa Michuzi Media Group Othman Michuzi yupo huko kuleta vitu hivi