Friday, September 27, 2013

MTANZANIA ACHAGULIWA KUWA RAIS WA KAMATI YA WATAALAM NA MAMENEJA YA AFRICA (UNI-AFRICA PROFESSIONALS & MANAGERS COMMITTEE) NA PIA MAKAMU RAIS WA DUNIA (UNI-GLOBAL PROFESSIONALS AND MANAGERS COMMITTEE)

Kwa mara nyingine bendera ya Tanzania imeendelea kupeperuka na kuwa juu baada ya Mtanzania Ndugu Francis Joseph Assenga (pichani) kuchaguliwa kushika Nyadhifa za Rais wa Kamati ya Wataalam na Mameneja ya UNI Africa katika Mkutano Mkuu wa Tatu wa Bara la Africa uliofanyika Nairobi, Kenya na kuhudhuriwa na Wajumbe 455 katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Jomo Kenyata (KICC) kuanzia tarehe 16 hadi 20 Septemba, 2013. 
Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Kazi na Hifadhi ya Jamii wa Kenya Mheshimiwa Samwel Kazungu Kambi kwa niaba ya Rais wa Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyata ambaye alipatwa na majukumu mengine. Katika Mkutano huo, mbali na kuchaguliwa kuwa Rais wa Afica ambayo Makao yake Makuu yako mjini Abdijan, nchini Ivory Coast.
Ndugu Assenga pia anakuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Wataalam na Mameneja ya Dunia (UNI Global Professionals & Managers) yenye Makao yake Makuu mjini Nyon, Switzerland. Ili kuchaguliwa kwa nyadhifa hizo, 
Ndugu Assenga alipendekezwa kwa pamoja na nchi za Ghana, Boukina Faso na Rwanda, na kuungwa mkono na nchi zote za Africa isipokuwa Senegal na Cameroun ambazo zilikuwa pia na wagombea wao katika nafasi hiyo. Aidha, Ndugu Assenga pia alichaguliwa kuwa Mjumbe Mwenza wa Kwanza wa Kamati ya Fedha ya UNI Africa. 
Ndugu Francis Assenga ambaye ataziongoza taasisi hizo kwa kipindi cha miaka minne hadi mwaka 2017 ni mtaalam mwenye taaluma mbali mbali za juu ambapo ana degree sita za fani tiofauti tofauti zikiwemo za Uchumi, Utawala wa Fedha, Uhasibu, Mipango, Uendeshaji wa Miradi na Sheria. Ndugu Assenga tayari amerejea nchini Tanzania akitokea Nairobi.
 Ndugu Francis Josseph Assenga (katikati) na Makamu wake Olasanoye Oyinkan wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa UNI Africa Professional & Managers kwenye Hoteli ya Hilton Mjini Nairobi
 Wagombea wa nafasi ya Urais na Umakamu Rais wa UNI Africa Professionals & Managers Committee wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya Uchaguzi kumalizika. Kutoka kushoto ni Pierre Louis Mouangue (Cameroun), Innocent Tsumbu (Afisa wa UNI Africa – Abdijan), Ulf Bengtsson (Sweden)-Rais wa UNI Global Professionals & Managers Committee), Francis Josseph Assenga (Tanzania) Olasanoye Oyinkan (Nigeria) na Ousmane Diagne (Senegal).
 Ndugu Francis Josseph Assenga (katikati) akihutubia kwenye Mkutamo Mkuu wa Tatu wa UNI Africa uliohudhuriwa na Wajumbe 455  kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Jomo Kenyata, Jijini Nairobi 
 Ndugu Francis Josseph Assenga (katikati) akihutubia kwenye Mkutamo Mkuu wa Tatu wa UNI Africa uliohudhuriwa na Wajumbe 455 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Jomo Kenyata, Jijini Nairobi 
 Ndugu Francis Josseph Assenga (kushoto) akipongezwa na Mwakilishi wa Rwanda Bwana Alexis  kwenye Mkutano wa Bara la Afrika wa Kamati ya Wataalam na Mameneja na Makamu wake Olasanoye Oyinkan wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Mkutano wa UNI Africa Professional & Managers kwenye Hotel ya Hilton Mjini Nairobi
 Ndugu Francis Josseph Assenga (katikati) akiwa na Wajumbe wenzake wa Mkutano Mkuu wa UNI Afrna nje ya Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Jomo Kenyata (KICC), Nairobi. Kulia kwake ni Ndugu Jonathan Peles (Tanzania) na Bwana Joe Kokella (Africa Kusini).
 Ndugu Francis Josseph Assenga (katikati) akishauriana jambo na Ndugu Jonathan Peles wa Tanzania wakati wa Mkutano. Kushoto kwao ni Mwakilishi mwingine wa Tanzania Bwana Samwel James Mgeni.
Ndugu Francis Josseph Assenga na Ndugu Jonathan Peles (wote kutoka Tanzania) wakifuatilia mada kwenye Mkutano Mkuu wa Tatu wa Bara la Afrika wa UNI Africa kwenye Ukumbi wa Kimamtaifa wa Mikutano wa Jomo Kenyata, Mjini Nairobi, Kenya.


No comments: