Tuesday, July 2, 2013

MKUTANO MKUU WA TANO WA WADAU WA MFUKO WA GEPF WAFANA MJINI ARUSHA

Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akifungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha. 
 Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Wiliam Erio akifuatilia mada wakati wa mkutano huo. 
Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daudi Msangi akifafanua jambo.
 Wadau.
 Mkurugenzi Masoko na Uendeshaji wa GEPF, Anselim Peter akitoa mada.
Meneja Masoko na Utekelezaji, Aloyce Ntukamazina.  
 Wadau wa mfuko wa GEPF.
 Baadhi ya wadau wakiwa katika mkutano huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa tano wa Mwaka wa wadau wa Mfuko wa akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), jijini Arusha.
Mkuu wa ICT-SSRA, Dk. Carina Wangwe. 
Mkurugenzi Masoko na Uendeshaji wa GEPF, Anselim Peter (kushoto) akibadilishana mawazo na Meneja Masoko na Utekelezaji, Aloyce Ntukamazina. 
 Baadhi ya wadau wakipata chai.
 Wanamuziki wa Marahaba Generation wakitumbuiza.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akifuatana na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi.
 Wasanii wa kikundi cha ngoma cha Watoto wa Simba cha jijini Arusha kikitumbuiza.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka akimsikili kwa makini Meneja Masoko na Utekeleza wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukamazina mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha. 
 Baadhi ya wadau wakifuatilia mkutano huo.
Mbunge wa Kigoma, Albert Obama akiwa na Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi katika mkutano huo.
 Wafanyakazi wa Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi Serikalini (GEPF) wakiwa wamepozi kwa picha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini, John Mongela akiagana na Meneja Masoko na Utekeleza wa Mfuko wa Akiba ya wafanyakazi Serikalini (GEPF), Aloyce Ntukamazina mara baada ya kufungua Mkutano Mkuu wa tano wa wadau wa mfuko huo ulifanyika jijini Arusha. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa GEPF, Daud Msangi, Mbunge wa Kigoma, Albert Obama na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Joyce Shaidi.
 Picha ya pamoja.

Na Mwandishi Wetu

Mifuko ya Hifadhi za Jamii imeaswa kuwekeza katika vitega uchumi vyenye tija ili mifuko hiyo iweze kuwa endelevu na kutoa huduma bora kwa watanzania.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Kazi na Ajira  Gaudencia Kabaka alipokuwa akizungumza katika mkutano wa 10 wa Mfuko wa Akiba ya  Wafanyakazi wa serikalini (GEPF) uliofanyika jijini hapa.

Gaudencia Kabaka alisema kuwa mifuko hiyo iwekeze zaidi katika vitega uchumi  ili kuepuka kufilisika na kuweza kujiendesha yenyewe kwa faida na kuwanufaisha wanachama wao.

Pia amewataka wananchi  kujiwekea akiba itakayowasaidia kukabiliana na majanga ya kiuchumi na kijamii yanayotokea katika maisha.

“Ni vizuri wananchi wakahamasishwa  kujiwekea akiba itakayowasaidia kipindi cha uzeeni,wanapokubwa na maradhi ama ulemavu kwasababu hatujui leo unaweza kuwa mzima una nguvu na kesho hauna nguvu ndio maana tunasema hatujui ya kesho unaweza kuwa mlemavu mtarajiwa ama marehemu mtarajiwa” alisema Waziri Kabaka.

Waziri kabaka ameitaka mifuko hiyo kuacha kugombania wanachama walioajiriwa tu badala yake wapanue wigo na kuwaendea watu  walioko katika sekta zisizo rasmi.

Naye mkurugenzi wa mfuko huo wa (GEPF), Daudi Msangi alisema kuwa  mfuko huo una lengo la kuhakikisha kuwa watu waliojiajiri wanaingia kwa wingi katika mfuko huo .

“Changamoto kubwa tuliyonayo ni wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha juu ya kuhusiana na mifuko ya jamii wengi wanadhani wanapoteza fedha jambo ambalo  halina  ukweli  bali  mifuko hiyo inawasaidia kujiwekea akiba kwa ajili ya sasa na ya  maisha ya badae”  Alisema Mkurugenzi  huyo.

No comments: