Friday, January 25, 2013

DKT. SHEIN AONGOZA WAUMINI WA KIISLAM KWENYE MAULID YA MTUME MUHAMMAD (S.A.W) VIWANJA VYA MAISARA,ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akitia ubani kama ishara ya ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Ustadh Abdulla Hamad wa Chuo cha Kiislamu,akitoa tafsiri ya Aya za Quran,zilizosomwa na Ustadh Rashid Jaffer wa Magogoni Mjini Zanzibar,akisoma Quran Tukufu ya Ufunguzi wa Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyosomwa jana katika Viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar,ambapo kila mwaka hufanyika Maulid kama hayo na kuhudhuriwa na maelfu ya Wumini wa Dini ya Kiislamu.
Mtafsiri Lugha kwa njia ya alama akitoa tafsiri ya maneno yanayozungumzwa wakati wa Hafla ya sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Wake za Viongozi na Akinamama wakisikiliza Maulid Barzanj ya Kuzaliwa kwa yaliyosomwa na wasomaji mbali mbali na Qasida katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu waliohudhuria katika sherehe za Maulid ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,(wa tatu kulia) akitiwa Marashi wakati wa kumswalia Mtume (S.A.W) wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa kwake katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akifuatana na Viongozi wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.
Ustadh Ali Twalib Mohamed,wa Kibanda Hatari Mjini Zanzibar akisoma Maulid Barzanj Mlango wa kwanza katika kusherehekea kwa kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana, na Rais Mstaafu wa Zanzibar Dk.Amani Abeid Karume,(katikati).
Wanafunzi wa Madrasa Munawara Shaurimoyo Wilaya ya Mjini Zanzibar wakisoma Qaswida ya Mwaka 1434 el Hijra,wakati wa sherehe ya Maulid ya Kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisra Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,iliyotayarishwa na jumuiya hiyo katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Mjini Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maulid EL Nabii Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis,alipowasili katika viwanja vya Maisara katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhamad (S.A.W) yaliyofanyika jana.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

No comments: