Sunday, October 28, 2012

HAFLA YA KUMUAGA KANAL MJENGWA DC MBINGA YAFANA SANA

Kutoka kushoto mkuu wa wilaya ya Nyasa Ernest Kahindi,mkuu wa wilaya ya mbinga mstaafu Kanal Edmund Mjengwa,mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Said Mwambungu,mkuu mpya wa wilaya Mbinga Senyi Ngaga na Mama Hanab Mwambungu wakigonga cheers wakati wa sherehe ya kumuaga Kanal Mjengwa jana mjini Mbinga.
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Mbinga Shaibu Mnunduma akigonganisha glass na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wakati wa sherehe ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa Wilaya hiyo Kanal mstaafu Edmund Mjengwa.
Askofu wa jimbo la Mbinga John Ndimbo akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu jana mjini Mbinga wakati wa sherehe ya kumuaga Mkuu wa zamani wa wilaya ya Mbinga kanal mstaafu Edmund Mjengwa mjini Mbinga.
Mkuu wa zamani wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Kanal mstaafu Edmund Mjengwa akizungumza jana mjini Mbinga wakati wa sherehe yake ya kumuaga,katikati mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na kulia mkuu mpya wa wilaya hiyo Senyi Ngaga.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akizungumza wakati wa sherehe ya kumuaga aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Mbinga kanal mstaafu Edmund Mjengwa,kulia mkuu wa wilaya ya Mbinga Senyi Ngaga na kushoto kanal Mjengwa.
Mkuu wa zamani wa wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma Kanal mstaafu Edmund akikata keki huku akishuhudiwa na mkuu mpya wa wilaya hiyo Senyi Ngaga kulia na mkuu wa wilaya mpya ya Nyasa Ernest Kahindi,wakati wa hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo.
Mkuu wa zamani wa wilaya Mbinga mkoani Ruvuma Kaanl mstaafu Edmund Mjengwa kulia akimlisha keki mkuu mpya wa wilaya hiyo Seniy Ngaga.
Mkuu mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu wa pili kulia na mkewe mama Hanab Mwambungu wakimpa zawadi kanal Mjengwa jana katika sherehe ya kumuaga Mjengwa mjini Mbinga.
Mkuu wa mkoa wa Said Mwambungu mbele jana,akiwaongoza wageni mbalimbali waliohudhuria hafla ya kumuaga mkuu wa zamani wa wilaya mbinga kanal mstaafu Edmund Mjengwa kucheza muziki.
Mkuu wa wilaya ya mbinga Senyi Ngaga kulia akicheza muziki na mkuu wa zamani wa wilaya hiyo Kanal mstaafu Edmund Mjengwa jana mjini Mbinga.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu na mkewe Hanab Mwambungu wakicheza muzik katika sherehe ya kumuaga kanl Mjengwa mjini mbinga.PICHA NA MUHIDIN AMRI

No comments: